WATU KADHAA WAHOFIWA KUKWAMA NDANI YA GHOROFA LILILOPOROMOKA


Watoto watatu wameokolewa baada ya jengo la ghorofa tatu lililokuwa katika ujenzi kuporomoka Sagana nchini Kenya.

Taarifa zinaonyesha kwamba jengo hilo liliporomoka siku ya Jumatatu, Juni 19,2023 jioni, na inaaminiwa kuwa wafanyakazi wa ujenzi kadhaa wamekwama ndani ya jengo hilo. 

Kwa mujibu wa ripoti ya Citizen TV, operesheni za kutafuta na kuokoa zilianza mara moja, na watu watatu waliokolewa kutoka kwenye vifusi baada ya tukio hilo. 

Watatu hao walipelekwa haraka katika Hospitali ya Murang'a Level Five kwa matibabu huku zoezi la kutafuta wenzao likiendelea hadi usiku wa manane.

Picha zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha umati wa watu waliokusanyika eneo la tukio, sehemu ya jengo ikiwa imepinduka upande mmoja huku ghorofa ya kwanza ikiwa imetapakaa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post