BENKI YA CRDB YADHAMINI MAADHIMISHO YA SIKU YA USHIRIKA DUNIANI TABORA


Kaimu Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi Ndg. Jumanne Wambura  Wagana akiuliza maswali kwa wateja waliotembelea banda la CRDB wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Ushirika Duniani.
Mkuu wa kitengo cha kilimo biashara wa benki ya CRDB, Shaban Maregesi akielezea jinsi CRDB ilivyochangia kwenye sekta ya kilimo mifugo na uvuvi na fursa mbalimbali zilipo CRDB mbele ya mgeni rasmi.
***

Benki ya CRDB imekuwa mdhamini mkuu wa Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani (SUD) kwa mwaka 2023. 

Akizungumza wakati wa Maadhimisho hayo bura  Wagana amesema hadi robo ya kwanza ya 2023, Benki ya CRDB imetoa mikopo ya kilimo yenye thamani ya TZS. 1.2 Trilioni, sawa na asilimia 43% ya mikopo yote ya kilimo nchini. Mikopo hiyo imesaidia Vyama vya Ushirika na AMCOS 472 kupata TZS. 494 Bilioni kwa ajili ya mazao makuu ya kimkakati.

 "Vilevile Benki ya CRDB imetoa mikopo kwenye sekta zingine za kiuchumi kama vile ufugaji, uvuvi, na ujenzi wa miundombinu. Kwa miaka mitano iliyopita, tumetoa mikopo ya TZS. 3.6 Trilioni kwenye sekta hizo",amesema Wagana. 

Amesema Benki ya CRDB pia imechangia mtaji wa TZS. 10.3 Bilioni kwa taasisi za Ushirika na kusaidia kuimarisha uongozi na utawala wao. 

"Huduma zote za benki zinapatikana kupitia mifumo ya kidigitali, na maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani kwa mwaka 2023 yanafanyika mkoani Tabora",ameongeza.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa benki ya CRDB Ndg. Joseline Kamuhanda pamoja na wafanyakazi wa CRDB wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mrisho Mpoto ( Mjomba ) ambae alitembelea banda la CRDB
Kaimu meneja wa kanda CRDB Kanda ya Magharibi Ndg. Jumanne Wambura Wagana akiteta jambo na mdau wa Ushirika Mh. Zainabu Telack ambae pia ni Mkuu wa mkoa wa Lindi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post