WAZAZI NA WALEZI WARUHUSUNI WATOTO KUJADILI YANAYOWAHUSU - SPIKA BUNGE LA WATOTO


Spika wa Bunge la Watoto wa mikoa ya Pwani na Dar es Salaam Isfahan Bungenyi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Bunge la Watoto wa mikoa hiyo, lililofanyika mkoani Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akizungumza wakati akifungua Bunge la watoto wa mikoa ya Dar es salaam na Pwani lililofanyika Jijini Dar es Salaam Juni 17, 2023, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amon Mpanju akieleza jambo wakati wa ufunguzi wa Bunge la Watoto wa mikoa ya Dar es salaam na Pwani, lililofanyika jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Dkt. Nandera Mhando akieleza lengo la kuanzishwa kwa Bunge la watoto, wakati wa ufunguzi wa Bunge la watoto wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani lililofanyika jijini Dar es salaam.
Wabunge wa Bunge la Watoto wa mikoa ya Dar es salaam na Pwani wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa ufunguzi wa Bunge hilo, mkoani Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis katika picha ya pamoja na wabunge wa Bunge la watoto wa mikoa ya Dar es salaam na Pwani lililofanyika Jijini Dar es Salaam , ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Wakili Amon Mpanju, kulia ni Kamshna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Nandera Mhando.

Na WMJJWM, DAR ES SALAAM

Spika wa Bunge la watoto wa Mikoa ya Dar es salaam na Pwani Isfahan Fakhru Bugenyi amewasihi Wazazi, Walezi, Serikali na watendaji nchini kuwatengenezea Watoto majukwa yatakayowawezesha kushiriki kikamilifu katika masuala yanayowahusu.

Bugenyi ameyasema hayo wakati wa Bunge la watoto wa Mikoa hiyo Juni 17, 2023 Jijini Dar es salaam, ambalo limelenga kuwakutanisha wadau, viongozi wa Serikali na Wizara za kisekta zinazohusika na masuala mbalimbali ya Watoto Ili kujua mahitaji na changamoto zao

Spika Bugeny amesema majukwaa hayo ni muhimu kwani yataiwezesha Serikali, wadau wa watoto, wazazi, walezi na watendaji kuzingatia kundi hilo wanapopanga mipango Sera, Sheria na Miongozo mbalimbali itakayosadifu mahitaji halisi na vipaumbele vya Watoto.

"Lengo la Bunge hili ni kuwatengenezea Watoto Jukwaa la ushiriki wa Siku ya Mtoto wa Afrika kikamilifu na pia kupaza sauti zao juu ya masuala yanayowahusu Ili kukuza uelewa wao na Jamii kwa ujumla juu ya Haki za Mtoto, Vilevile Bunge la watoto linalenga kuwakutanisha viongozi wa Serikali, Wizara yenye dhamana na Watoto Ili wasikie mahitaji na changamoto za Watoto Ili wanapo panga mipango na sera, sheria na Miongozo mbalimbali iendane mahitaji halisi na vipaumbele vya Watoto"

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ally Khamis ambaye ambaye ameshiriki ufunguzi wa Bunge hilo amemtaka Mkurugenzi wa Idara ya Watoto wa Wizara hiyo kushiirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Wizara ya elimu kuhakikisha kila shule inakuwa na Bunge la watoto.

"Tukiwa kwenye shule tunaweza kutafuta kila shule wagombea na kuweza kufanya Bunge la kitaifa na tukalifanya Bunge la Serikali ya watoto na Bunge ilo litawanufaifa watoto wenyewe kijitambua na kujieleza na kuibua changamoto za ukatili na kama kutakuwa na uelewa huu basi tutatokomeza ukatili" amesema Mwanaidi

Mhe Mwanaidi akatumia fursa hiyo kugusia juu ya suala la watoto na Sheria ya ndoa za utotoni.

"Serikali ya awamu ya sita inayo ongozwa na Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanza kurekebisha vifungu vya sheria ya ndoa taratibu zinaendelea kufanyika kujua umri gani mtoto anatakiwa kuolewa na Umri gani mtoto atakiwi kuolewa" aliongeza Mhe. Mwanaidi.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Wakili Amoni Mpanju amewaasa watoto, kutumia fursa za kielimu wanazopewa kama silaha dhidi ya vitendo vya ukatili katika jamii zao Huku Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la LHRC Dkt. Anna Henga Akisema Bunge hili la watoto ni sehemu ya kupaza sauti zao na kujadili mambo yanayo wahusu watoto wenyewe.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post