Picha : RC MNDEME AKUTANA NA MACHINGA...SAKATA LA BANDARI MOTOO!! "SHINYANGA HATUDANGANYIKI"

Mkuu wa  Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na Machinga mkoa  wa Shinyanga kupitia Shirikisho la Umoja wa Machinga Mkoa wa Shinyanga na Taifa.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa `Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amekutana na kuzungumza na wajasiriamali wadogo mkoa wa Shinyanga kupitia Shirikisho la Umoja wa Machinga Mkoa wa Shinyanga ambapo ametumia fursa kutoa ufafanuzi kuhusu azimio la kuridhia Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kupitia Kampuni yake ya DP World kuhusu Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi wa Bandari Tanzania huku Machinga wakiunga mkono suala la uwekezaji katika Bandari.

Mkutano huo umefanyika leo Jumatatu Juni 19,2023 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambapo wajasiriamali hao wadogo na viongozi wao ngazi ya Mkoa na taifa wamehudhuria mkutano huo.

Akizungumzia kuhusu azimio la kuridhia Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kupitia Kampuni yake ya DP World kuhusu Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi wa Bandari Tanzania, Mkuu huyo wa Mkoa amesema Mkataba huo una manufaa makubwa katika mkoa wa Shinyanga na taifa kwa ujumla kwa sababu mkoa wa Shinyanga upo jirani na masoko ya nchi jirani.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na Machinga

“Sisi Shinyanga ni lango la kiuchumi, uwekazaji haukuanza leo, kwanini watu wanapotosha kwa malengo gani?, Rais wetu ni Mzalendo, tumuache afanye kazi, tusifanye upotoshaji”,amesema Mndeme.

Amesema kutokana na kwamba Kampuni ya DP World kwa kuzingatia uzoefu wake katika uendeshaji wa shughuli za bandari barani Afrika, Asia, Ulaya na Amerika ya Kaskazini na Kusini,Uwekezaji huo katika Bandari ya Dar es salaam utaleta manufaa katika kupunguza muda wa meli kukaa nangani kutoka siku 5 mpaka masaa 24 na kupunguza gharama za utumiaji wa Bandari na kufungua masoko ya kimkakati katika eneo la bidhaa na biashara ya usafirishaji ndani ya nchi na kanda jirani.

“Shinyanga hatudanganyiki, Machinga hatudanganyiki, tunataka bidhaa zije kwa spidi. Rais wetu anania nzuri ya kutaka bidhaa ziwahi kuja machinga wapate bidhaa wauze, wanataka kutukatisha tamaa, hili halikubaliki. Haiwekezani tumkatishe tamaa Rais wetu”,ameongeza Mndeme.

Mndeme amesema serikali inaendelea kushirikiana na Machinga katika kuliletea maendeleo taifa hivyo kuwaomba wafanyabiashara hao kuepuka kutumiwa vibaya na watu wasioitakia mema nchi ya Tanzania.

Masoko yanaendelea kujengwa na sasa hivi hakuna biashara hazifungwi. Mhe. Rais Samia ameleta shilingi Bilioni 612 kwa ajili ya maendeleo mkoani Shinyanga. Naomba msikubali kutumika na watu wasiotutakia mema,wenye nia mbaya. Tumuunge mkono Mhe. Rais Samia, Amani yetu tusiivuruge”,amesema Mndeme.
“Kama mtu anataka ugomvi na mimi akamate machinga, atakuwa haki yangu, fuateni sharia na taratibu za kufanya biashara. Nyie Machinga wa mkoa wa Shinyanga mnajielewa vizuri, mna hofu ya Mungu. Nawaahidi hakuna machinga atakayesumbuliwa Shinyanga, serikali ipo pamoja na nyinyi ilimradi mnazingatia sheria”,amesema Mndeme.

“Niwaombe katika masoko yetu, tutaweka sehemu kwa ajili ya faragha ya wanawake kunyonyesha watoto, anafanya biashara lakini pia mtoto naye anapata haki yake”,ameongeza.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wafanyabiashara kuwa mstari wa mbele kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Akisoma tamko la  Umoja wa wafanyabiashara ndogondogo (Machinga)  Mkoa wa Shinyanga kuhusu mapendekezo ya kuridhia mkataba baina ya serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya kuendeleza na kuboresha utendaji kazi wa Bandari Tanzania , Mwenyekiti wa Shirikisho Mkoa wa Shinyanga Boniphace Petro amesema wameridhia azimio hilo kwa maslahi ya taifa.

"Tumepokea maelezo ya awali kuhusu mapendekezo ya kuridhia Mkataba baina ya serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendeshaji  na uboreshaji  kazi wa Bandari Tanzania. Mhe. Mkuu wa Mkoa ametupitisha katika maelezo ya mapendekezo ya kuridhia mkataba na tumeelewa lengo la serikali ni jema kwani serikali inapambana kutuletea maendeleo katika nchi yetu",amesema Mwenyekiti huo wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Mkoa wa Shinyanga.

"Sisi Machinga Mkoa wa Shinyanga tunabariki na kuridhia makubaliano ya Uwekezaji katika bandari huku tukilaani vikali wale wanaokosoa makubaliano na kupotosha jamii kwa uchochezi wa maneno yasiyo na tija. Tunaahidi kuwa mabalozi wema katika maeneo yetu na tutakuwa sehemu ya wanaoelezea kwa nia njema juhudi za maendeleo zinazofanywa na Serikali katika nchi yetu. Tunatanguliza shukrani zetu kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutupambania na kutuletea maendeleo  katika mkoa wetu na nchi yetu kwa ujumla”,amesema.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na wajasiriamali wadogo mkoa  wa Shinyanga kupitia Shirikisho la Umoja wa Machinga Mkoa wa Shinyanga na Taifa. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na wajasiriamali wadogo mkoa wa Shinyanga kupitia Shirikisho la Umoja wa Machinga Mkoa wa Shinyanga na Taifa.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Mkoa wa Shinyanga Boniphace Petro akisoma tamko
Mwenyekiti wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Mkoa wa Shinyanga Boniphace Petro akisoma tamko
Mwenyekiti wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Mkoa wa Shinyanga Boniphace Petro akisoma tamko
Wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post