WADAU WAPEWA ELIMU KUHUSU UMUHIMU WA KUTAMBUA SHERIA, KANUNI ZINAZOONGOZA DIGITALI NCHINI
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya The Launch Pad Tanzania, Carol Ndosi akizungumza wakati wa Warsha ya kujenga uelewa kuhusu Sheria, Sera na Kanuni zinazosimamia Masuala ya Kidigitali Nchini Tanzania na kuwezesha majadiliano ya changamoto na fursa zilizopo katika Hoteli ya Protea, Dar es Salaam, Mei 30, 2023 ikiwa imeandaliwa na Shirikisho la Wadau Wanaotetea Haki za Kidigitali Tanzania (Digital Rights Coalition).

Meneja Programu wa Asasi ya Kiraia ya Jamii Forums, Ziada Seukindo akizungumza wakati wa Warsha ya kujenga uelewa kuhusu Sheria, Sera na Kanuni zinazosimamia Masuala ya Kidigitali Nchini #Tanzania na kuwezesha majadiliano ya changamoto na fursa zilizopo katika Hoteli ya Protea, Dar es Salaam, Mei 30, 2023 ikiwa imeandaliwa na Shirikisho la Wadau Wanaotetea Haki za Kidigitali Tanzania (Digital Rights Coalition).Wadau wakitoa maoni katika Warsha ya kujenga uelewa kuhusu Sheria, Sera na Kanuni zinazosimamia Masuala ya Kidigitali Tanzania pamoja na kuwezesha majadiliano ya changamoto na fursa zilizopo, waandaaji ni Shirikisho la Wadau Wanaotetea Haki za Kidigitali Tanzania (Digital Rights Coalition), imefanyika kwenye Hoteli ya Protea Jijini Dar es Salaam, Mei 30, 2023.
***


Imeelezwa kuwa uelewa wa baadhi ya Watanzania bado ni mdogo kuhusu Sheria za Kidigitali hali ambayo imechangia kutokea kwa makosa mengi, hivyo juhudi za ziada zinahitaji kuchukuliwa ili kufikisha elimu hiyo.


Hayo yameelezwa leo Meo 30, 2023 Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya The Launch Pad, Carol Ndosi, katika Warsha ya kujenga uelewa kwa Wadau wa Digitali kuhusu Sheria, Sera na Kanuni zinazosimamia Masuala ya Kidigitali Nchini Tanzania pamoja na kuwezesha majadiliano ya changamoto na fursa zilizopo, ambayo imefanyika katika Hoteli ya Protea Jijini Dar es Salaam, Mei 30, 2023.


Ndosi amesema Kampuni za Simu zinaweza kutoa elimu kwa watumiaji hususani wakati mtu anavyonunua laini ya simu na wakati akiwasha simu apate andiko fupi linalomjuza kuhusu Sheria, jinsi ya kujilinda Mtandaoni na pale ambapo anapitia unyanyasaji, wizi anaweza kwenda kuripoti wapi.


Kwa upande wake Meneja Programu wa Jamii Forums, Ziada Seukindo amesema kuwa lengo la Warsha hiyo ni kujenga uelewa kwa Wadau kuhusu Sheria, Sera na Kanuni zinazosimamia Masuala ya Kidigitali nchini Tanzania pamoja na kuwezesha majadiliano ya changamoto na fursa zilizopo.


Baadhi ya Taasisi zilizoshiriki ni The Launch Pad Tanzania, TGNP, TAMWA, Twaweza, Nukta Africa, HakiElimu, Chuo cha Aga Khan, Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (WiLDAF), Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), UTPC, Pollicy, Tai Tanzania, Her Initiative na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post