UIMARISHWAJI WA TVLA UNAENDA KUSAIDIA KUIMARIKA KWA MIFUGO NCHINI KUWEZA KUPATA MASOKO NJE YA NCHI-PROF.SHEMDOE

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe akimsikiliza Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Magonjwa na Usimamizi Viwango vya Ubora-TVLA, Bw. Zachariah Makondo wakati akitembelea maabara za Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) leo Mei 12,2023 Jijini Dar es Salaam.
****************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe amefanya ziara kutembelea Maabara za Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kufahamu na kujionea kazi ambazo zinafanywa na Wakala hiyo.

Akizungumza wakati wa Ziara yake leo Mei 12, 2023 Jijini Dar es Salaam, Prof. Shemdoe amesema uimarishwaji wa TVLA unaenda kusaidia kuimarika kwa mifugo nchini na kuweza kupata masoko mengi nje ya nchi.

Amesema TVLA wamekuwa wakifanya maandalizi ya utengenezaji wa chanjo mbalimbali za mifugo ambazo zinasaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia maambukizi ya magonjwa mbalimbali kwenye mifugo.

"Miaka michache iliyopita tulikuwa tunapeleka nyama nje ya nchi tani elfu moja, lakini sasa mwaka huu ambao tunamalizia mwaka wa fedha tayari tumeshavuka tani elfu 12, kwahiyo tunapoelekea ni mahala pazuri". Amesema Prof. Shemdoe.

Aidha amewapongeza TVLA kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya ikiwemo kutambua magonjwa ya mifugo ambayo yapo nchini ili kuweza kuyazuia na kuyatokomeza.

Pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha ambazo zimesaidia kuimarisha TVLA na kuweza kufanya kazi kwa weledi mkubwa katika kuhakikisha wanadhibiti magonjwa ya mifugo.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Stella Bitanyi amesema kuwa wanategemea kwa kiasi kikubwa ziara ya Katibu Mkuu kuzaa matunda kwani ameona ni kwa namna gani TVLA wamekuwa wakijtahidi kuhakikisha inafanya vizuri katika kutekeleza majukumu yake.

Pamoja na hayo amemuhakikishia Katibu Mkuu kuwa wataendelea kufanya kazi kwa weledi zaidi katika kuhakikisha wanadhibiti magonjwa ya mifugo nchini.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Stella Bitanyi mara baada ya kuwasili na kutembelea katika Ofisi za TVLA leo Mei 12,2023 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe akisalimiana na Mkuu wa Maabara ya Magonjwa ya kuambukiza ya Wanyana na Teknolojia TVLA, Dkt. Jelly Chang'a i mara baada ya kuwasili na kutembelea katika Ofisi za TVLA leo Mei 12,2023 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe akisalimiana na Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Magonjwa na Usimamizi Viwango vya Ubora-TVLA, Bw. Zachariah Makondo mara baada ya kuwasili na kutembelea katika Ofisi za Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) leo Mei 12,2023 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe akizungumza na watumishi wa Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) baada ya kuwasili na kutembelea katika Ofisi za TVLA leo Mei 12,2023 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea ofisi za Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) leo Mei 12,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Stella Bitanyi akielezea majukumu yanayofanywa na TVLA mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe ambaye ametembelea Ofisi na Maabara za TVLA leo Mei 12,2023 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe akimsikiliza Mkuu wa Idara ya Maabara ya Vyakula vya Mifugo TVLA Dkt. Scholastica Dotto wakati akitembelea maabara za Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) leo Mei 12,2023 Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe akimsikiliza Afisa Mtafiti wa Mifugo-TVLA, Bi. Evaline Mfuru wakati akitembelea maabara za Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) leo Mei 12,2023 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe akizungumza jambo na Afisa Mtafiti wa Chakula cha Mifugo TVLA, Bw. Henry Mrundachuma wakati akitembelea maabara za Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) leo Mei 12,2023 Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Bakteria TVLA Bw. Godwin Minga wakati akitembelea maabara za Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) leo Mei 12,2023 Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe akimsikiliza Mkuu wa Maabara ya Magonjwa ya kuambukiza ya Wanyana na Teknolojia TVLA Dkt. Jelly Chang'a wakati akitembelea maabara za Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) leo Mei 12,2023 Jijini Dar es Salaam.


(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post