TTCL YANG’ARA MAONESHO YA WADAU WA MAWASILIANO VIWANJA VYA BUNGE DODOMA



SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dk Tulia Ackson,akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL),Mhandisi Peter Ulanga wakati alipotembelea banda la Shirika hilo katika Maonesho yanayoendelea viwanja vya Bunge Jijini Dodoma leo Mei 18,2023.Kushoto ni Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Mathew Kundo.


SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dk Tulia Ackson,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua mabanda mbalimbali katika Maonesho yanayoendelea viwanja vya Bunge Jijini Dodoma leo Mei 18,2023.


Meneja Biashara TTCL Dodoma Bi.Leyla Pongwe,akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la shirika hilo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL),Mhandisi Peter Ulanga wakati katika Maonesho yanayoendelea viwanja vya Bunge Jijini Dodoma leo Mei 18,2023.



Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) imeendelea na maonesho ya baadhi ya Huduma na bidhaa wanazotoa ambapo waheshimiwa wabunge na viongoz mbali mbali wamejitokeza katika banda la shirika hilo kwa Lengo ni kujionea utendaji kazi wake. SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dk Tulia Ackson leo Mei 18,2023 alitembelea banda la TTCL viwanjani hapo na kulipongeza Shirika hilo kwa kuweza kufanikisha huduma za mawasiliano ya intaneti kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Spika Tulia amesema suala la mkongo kufika nyumbani ni jambo la muhimu kwani matumizi ya data na teknolojia ni muhimu.

“Nitume nafasi hii kuwapongeza TTCL kwa kutuleta huduma hii naamini zitapunguza gharama ya matumizi ya bando ambayo tumekuwa tunalalamika.

“Tumeona mmefika Kilimanjaro,hiyo itakuwa nzuri kwa sababu kutakuwa hakuna uongo uongo,piga tujue umefika kileleni kama mmefika pale ni vizuri nawaongeza sana mnafanya kazi nzuri,”amesema Spika Tulia.

Kwa upande wake Meneja Biashara TTCL Dodoma Bi.Leyla Pongwe amesema wamefika bungeni kuwaonesha wabunge mikakati ambayo wanayo katika kuisaidia serikali kwenye kuchagiza kufikia uchumi wa kidigital mpaka mwaka 2025.

Amesema wanajivunia kwa sasa kwani wameweza kufikisha huduma ya intaneti katika mlima Kilimanjaro.

“Zamani ilikuwa mtalii akipanda juu anakuwa hapatikanai ila sasa hivi mtalii anapatikana.Sasa hivi tunamletea mtanzania fiber mpaka nyumbani kwake analipia kifurushi kwa mwezi kwani ili kufikia uchumi wa kati lazima uwe na intaneti,”amesema

Maonesho ya wadau wa Mawasiliano yanaendelea kwa siku 3 katika viwanja vya bunge ikiwa ni kuelekea kwenye bunge la bajeti ya Mawasiliano linalotarajiwa kusomwa kesho na Waziri wa Habari na Mawasiliano Mheshimiwa Nape Mnauye.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments