BAA NA KUMBI ZA STAREHE 89 ZAFUNGWA KISA KELELE TANZANIA

Mkurugenzi Mkuu wa Bazara la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 8,2023 Jijini Dar es Salaam katika kikao cha mrejesho wa operesheni ya msako wa kubaini baa na kumbi za starehe zinazopiga kelele zilizozidi kiwango.

***************

Bazara la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limezifungia baa na kumbi za starehe 89 katika mikoa mitatu ikiwemo Mkoa wa Dar es salaam, kwa kupiga kelele zinazozidi viwango kinyume cha sheria ya mazingira ya mwaka 2014.

Akizungumza leo Mei 8,2023 Jijini Dar es salaam kwenye kikao cha mrejesho wa operesheni ya msako wa kubaini baa na kumbi za starehe zinazopiga kelele zilizozidi kiwango, Mkurugenzi Mkuu NEMC Dkt. Samuel Gwamaka amesema wamefikia hatua hiyo kutokana na maeneo hayo ya biashara kupiga kelele na mitetemo iliyozidi viwango.

Amesema mpaka wamefikia uamuzi huo wa kuwafungia ni kwa sababu sio mara ya kwanza kwa kumbi hizo kufanya makosa hayo, licha ya NEMC kuwaonya kwa nyakati tofauti lakini hawakuweza kufuata utaratibu.

"Hatupendi kufungia kazi zenu lakini inatupasa tufanye hivyo kama hamuwezi kufuata utaratibu uliowekwa, tunajua mnalipa kodi pia mmetoa ajira kwa vijana lakini mnapovunja sheria na utaratibu lazima tuwachukulie hatua". Amesema Dkt.Gwamaka

Akizungumza kwa niaba ya walimiliki wa baa Nina John, ameiomba NEMC kuwapunguzia adhabu walizowapa maana ni kubwa na kwasasa wapo tayari kutii sheria kuhusu kudhibiti kelele zilizozidi viwango.

Hadi sasa Baraza hilo limezifungia baa na nyumba za starehe 78 Jijini Dar es salaam, tano Dodoma sita katika mkoa wa Mwanza na kuweka masharti matatu ikiwemo kufunga vifaa vya kudhibiti kelele na kulipa faini ya milioni tano kwa wale waliowahi kuonywa na milioni mbili wa wafanyabiashara wapya.
Mkurugenzi Mkuu wa Bazara la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 8,2023 Jijini Dar es Salaam katika kikao cha mrejesho wa operesheni ya msako wa kubaini baa na kumbi za starehe zinazopiga kelele zilizozidi kiwango.

Mkurugenzi Mkuu wa Bazara la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 8,2023 Jijini Dar es Salaam katika kikao cha mrejesho wa operesheni ya msako wa kubaini baa na kumbi za starehe zinazopiga kelele zilizozidi kiwango.


Baadhi ya Watumishi wa Bazara la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu NEMC Dkt.Samuel Gwamaka katika kikao cha mrejesho wa operesheni ya msako wa kubaini baa na kumbi za starehe zinazopiga kelele zilizozidi kiwango.



(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post