MKUU WA WILAYA YA BAGAMOYO AWAFAGILIA WATUMISHI CHALINZE


NA ELISANTE KINDULU, CHALINZE-

MKUU wa wilaya ya Bagamoyo ,Bi Halima Okash amewapongeza watumishi wa halmashauri ya Chalinze kwa kuonyesha mshikamano katika zoezi la mapokezi ya mwenge wa uhuru yaliyofanyika siku chache zilizopita.


Mkuu huyo wa wilaya alitoa sifa hizo alipokutana na baadhi ya watumishi hao katika mkutano maalum mjini hapa.


Mkuu huyo wa Wilaya ya Bagamoyo alisema kuwa watumishi na wakazi wa Halmashauri ya Chalinze walijitokeza kwa wingi na kuonyesha umoja na mshikamano katika mapokezi ya mwenge wa uhuru kwa Mwaka huu .


Aidha Mheshimiwa Okash aliwataka watumishi kuendeleza mshikamano huo katika masuala mbalimbali ya maendeleo katika ustawi wa Chalinze na Taifa kwa ujumla.


Wakati huo huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze Bw. Ramadhani Possi alipokea pongezi hizo kwa niaba ya watumishi hao na kuahidi ushirikiano zaidi kwa maslahi ya umma.

Halmshauri ya Chalinze ni moja ya Halmashauri katika Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post