KATAMBI AFAFANUA MFUMO WA KUWALIPA KIINUA MGONGO WAZEE



Na Mwandishi Wetu, DODOMA

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amesema serikali inazingatia watanzania wote wanaojenga nchi yao na imeweka utaratibu wa kupata pensheni kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa waajiriwa na waliopo kwenye sekta isiyo rasmi.

Mhe.Katambi ameyasema hayo Mei 2, 2023 bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Magu (CCM), Mhe. Boniventura Kiswaga ambaye amehoji lini serikali italipa kiinua mgongo kwa wazee ambao hawajawahi kuajiriwa.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Katambi amesema kiinua mgongo ni malipo ambayo hulipwa na mwajiri pindi mfanyakazi wake anapostaafu kufanya kazi.

Mhe. Katambi amefafanua kuwa, kutokana na kuwepo kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii mwajiriwa na mwajiri huchangia, mfanyakazi hulipwa pensheni badala ya kiinua mgongo na hupokea mafao ya mkupuo mara anapostaafu na baadae kuendelea kulipwa pensheni ya kila mwezi kwa maisha yake yote na kwasasa hakuna mfumo wa kulipa kiinua mgongo kwa wazee ambao hajawahi kuajiriwa.

Hata hivyo, amesema kwa watu waliopo kwenye sekta isiyo rasmi ikiwamo wajasiriamali, wakulima na wafugaji, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) ndio wenye jukumu la kushughulikia sekta hiyo na umeanza kukusanya michango kwa kuwatambua waliyo kwenye makundi hayo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments