DKT ANDILILE ATOA ELIMU YA UDHIBITI WIKI YA NISHATI DODOMA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).Dkt. James Andilile (watatu kulia) akizungumza jambo na Kamishna wa Mafuta na Gesi, Bw. Michael Mjinja( wa tano kutoka kulia) leo Mei 30,2023 alipotembelea Banda la EWURA katika maonesho ya Wiki ya Nishati yanayoendelea katika viwanja vya Bunge la Tanzania, jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).Dkt. James Andilile ( wa nne kutoka kulia) akiteta na Waziri wa Nishati( wa tatu kulia) Mhe. January Makamba, katika viwanja vya Bunge ambapo maadhimisho ya Wiki ya Nishati yanaendelea.Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Bw. Maharage Chande.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).Dkt. James Andilile,( kulia) akimkabidhi Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe( kushoto) mkoba wa EWURA, wakati Waziri huyo alipotembelea banda la EWURA kwenye maonesho ya Wiki ya Nishati, viwanja vya Bunge Dodoma leo Mei 30,2023.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).Dkt. James Andilile (Kushoto) akimkabidhi mkoba wa EWURA, Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, Mheshimiwa George Simbachawene alipotembelea banda la EWURA, kwenye Maonesho ya Wiki ya Nishati yanayofanyika katika Viwanja vya Bunge, Dodoma, leo Mei 30,2023.

Na.Mwandishi Wetu-DODOMA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).Dkt. James Andilile, leo 30 Mei 2023, ameshiriki kutoa elimu ya udhibiti wa huduma za nishati katika maonesho ya Wiki ya Nishati yanayoendelea katika viwanja vya Bunge, jijini Dodoma.

Dkt Andilile amewaelimisha wadau mbalimbali waliotembelea banda la EWURA kuhusu utaratibu wa kupata leseni za umeme, shughuli za petroli na gesi asilia pamoja na namna ya kuwasilisha malalamiko yanayohusu huduma zinazodhibitiwa; sanjari na namna EWURA ilivyorahisisha masharti ya leseni za vituo vya mafuta maeneo ya vijijini ili wananchi wa maeneo hayo wapate huduma hiyo kwa urahisi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post