Jonathan Jacob Meijer (41) raia wa Uholanzi amepigwa marufuku kusambaza mbegu zake za kiume baada ya kugundulika kuwa ana watoto zaidi ya 550 duniani kupitia utoaji wa msaada wa mbegu za kiume za uzazi.
Mwanaume huyo mwaka 2017 alizuiwa kutoa mbegu za uzazi kwenye kliniki ya masuala ya uzazi nchini Uholanzi baada ya kufahamika kuwa alikuwa amezalisha watoto zaidi ya 100
Inaelezwa kuwa badala ya kuacha kuendelea na utoaji wa msaada huo, Jonathan aliendelea kutoa mbegu zake nje ya nchi yake na kwa njia ya mtandao.
Mahakama ya Uholanzi mjini The Hague imemwambia atoe orodha ya kliniki zote alizowatumia na kuziagiza ziharibu mbegu zake.