TCRA YAZISHAURI MALULA TV, DELLAH ONLINE TV & MISALABA BLOG ZIJISAJILI.... DC SAMIZI ATAKA WAANDISHI WATUMIE VIZURI KALAMU ZAO

                    
                   Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC) imeadhimisha Siku ya uhuru wa vyombo vya habari
'World Press Freedom Day' kwa kufanya mkutano na wadau wa vyombo vya habari mkoa wa Shinyanga.


Maadhimisho hayo yamefanyika leo Alhamisi Mei 18,2023 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme.


Mhe. Samizi amewapongeza waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga kwa kazi nzuri wanayofanya katika utekelezaji wa majukumu yao huku akiwataka kutumia kalamu zao za vizuri.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi

“Wito wangu kwa waandishi wa habari tutumie kalamu zetu na matamshi yetu katika kuhabarisha ili habari iliyokusudiwa ifike kwa maksudi yaliyokusudiwa ikiwemo kuhabarisha na kuburudisha”,amesema Samizi.


“Nitoe rai kwa watu wanaopenda uandishi wa habari watambue kuwa uandishi wa habari ni taaluma siyo utashi tu wa kuandika hivyo kama wanamatamanio ya kuwa waandishi wa habari basi waende darasani kusoma”,ameongeza Mhe. Samizi.

Mkuu huyo wa wilaya amewataka maafisa habari kushirikiana na waandishi wa habari na kuhakikisha wanachukua na kuzishughulikia changamoto zinazowakabili huku akisisitiza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na vyombo vya habari katika shughuli mbalimbali.

Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo amewataka watoa huduma za maudhui kuhakikisha wanazingatia sheria na kuwa na leseni za utoaji huduma za mawasiliano akisisitiza kuwa hataruhusu sheria zivunjwe.
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya ziwa Mhandisi Francis Mihayo

“Niwaombe wale ambao wana Blogs na Online Tv ambazo hazina leseni muombe leseni, andikeni vizuri vichwa vya habari vizuri. Unakuta mtu hajasomea uandishi wa habari , hana taaluma na hawa leseni ya TCRA lakini anatoa huduma za maudhui mtandaoni, acheni hayo”,amesema Mihayo.


“Lakini hivi sasa tuna wimbi la ku Copy na Ku Paste, unakuta habari imekosewa imesambaa kila chombo cha habari ikiwa na makosa yale yale, kuweni makini lakini pia nendeni shule mkaongeze ujuzi kwani sheria inawataka msome. Hakikisheni mnazingatia sheria na mnafuata sheria”,amesema Mihayo.


“Waandishi wa habari msichanganye uandishi wa habari na siasa, uanaharakati. Kama unataka uanaharakati achana na uandishi wa habari, kama unataka siasa jipambanue achana na uandishi wa habari. Chagua unataka kuwa mwanasiasa, mwanaharakati au mwandishi wa habari”,amesema Mhandisi Mihayo.

Meneja huyo wa TCRA Kanda ya Ziwa  pia amewataka waandishi wa habari kuandika habari zenye tija na kuandika vichwa vya habari vinavyoendana na maadili ya uandishi wa habari.

Mhandisi Mihayo ametumia fursa hizo kuziagiza baadhi ya Blogs na Online TV ikiwemo Dellah Online Tv, Misalaba Blog na Malula TV kusitisha mara moja huduma za utoaji maudhui mtandaoni mpaka pale watakapopata leseni kutoka TCRA.

“Kuanzia leo Dellah Online Tv, Malula Tv na Misalaba blog na wengine wote wanaotoa huduma za maudhui mtandaoni bila leseni wasitisishe shughuli za kuchapisha habari. Kwanini mnanichokoza? Kuanzia sasa naagiza msitishe uchapishaji wa habari kwenye mitandao yenu mpaka pale mtakapopata leseni kutoka TCRA”, amesema Mhandisi Mihayo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru ameiomba serikali kuwapa magari mazuri waandishi wa habari wakati wa ziara za viongozi kwani kumekuwa na tabia ya waandishi wa habari kupewa magari mabovu.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya uhuru wa vyombo vya habari wa Shinyanga leo Alhamisi Mei 18,2023
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya uhuru wa vyombo vya habari mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Mei 18,2023
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Mei 18,2023
 Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Mei 18,2023
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya  Uhuru wa Vyombo vya habari mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Mei 18,2023
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Mei 18,2023
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari  mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Mei 18,2023
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari  mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Mei 18,2023
Katibu wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Ali Lityawi akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari  mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Mei 18,2023
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments