MREMBO AUAWA KWA KUPIGWA MPINI NA MUMEWE KISA 'KUKATA MAUNO' SANA


Picha haihusiani na habari hapa chini
 ***
Kitendo cha kucheza nyimbo kwa mtindo wa kunengua (Twerking) kimemsababishia umauti Silvia Nachula mwenye umri wa miaka 32 kwa kupigwa hadi kufa na mume wake.


Tukio hilo limetokea huko mji wa Kabwe uliopo katikati ya Zambia, tovuti ya Zambian Observer ya nchini humo imeripoti.

Inadaiwa mume wake aitwaye Gift Hamunyati (42), mwenye wake wawili aliwachukua wake zake hao na kwenda nao baa akiwemo Nachula ambaye kwa sasa ni marehemu.


Hata hivyo, wakati unywaji pombe ukiendelea, Nachula alikuwa akinengua na kukatika kitu ambacho hakikumfurahisha Hamunyati, ndipo alipomshushia kipigo kikihusisha mpini wa shoka baada ya kutoka nje ya baa hiyo.


Kamishna wa Polisi wa Mkoa wa Kati, David Chileshe ambaye amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kusikitisha amasema lilitokea jana majira ya saa saba usiku.


“Ukweli ni kwamba mwanaume huyo alienda kulewa na wake zake wawili na akakasirishwa na jinsi mkewe aliyefariki alivyokuwa akijivinjari. Walipotoka waligombana hivyo kumvamia na mpini wa shoka,” amesema Chileshe.


Amesema marehemu alivunjika taya ya juu, aliharibiwa sehemu kubwa ya paji la uso, kichwa, shavu na kukatwa kwenye sehemu yake ya siri.


"Mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu ya Kabwe ukisubiri uchunguzi. Mke wa pili alifanikiwa kutoroka baada yeye kuanza kushambuliwa alipojaribu kuingilia ugomvi kumwokoa mke mwenza,” amemalizia Chileshe.


Imeandaliwa na Sute Kamwelwe.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

1/Post a Comment/Comments

Post a Comment