MBUNGE DEUS SANGU AONGOZA SHEREHE ZA KUMPONGEZA RAIS SAMIA BAADA YA UJENZI WA SHULE ILIYOGHARIMU ZAIDI MIL.670


Mbunge wa jimbo la Kwela Mhe. Deus Sangu amempongeza Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha ujenzi wa shule mpya ya sekondari ambayo itaondoa adha ya watoto kutembea umbali mrefu.

Sangu ameyasema hayo Tarehe 06/07/2023 wakati wa sherehe maalum ya kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan zilizofanyika katika kata ya Nankanga Mkoani rukwa.


Katika sherehe hizo Mhe. Deus Sangu aliambatana na Mhe. Venant Protas Mbunge wa jimbo la Igalula mkoani Tabora Mhe. Sangu amesema "Mhe. Rais ametupa heshima kubwa wana Nankanga kwa kutupatia fedha zaidi ya milioni 470 kujenga shule hii na ameahidi kutuongezea sh milion 150 ili kukamilisha kabisa shule hiii na sasa imefunguliwa watoto zaidi ya 270 wameanza masomo, kufanya sherehe hii ni salamu kwa Mhe. Rais Dkt. Samia. 

Natoa rai kwa wazazi, Walezi kuongeza msukumo wa elimu kwa watoto wenu, ili kuepukana na adha za mimba za utotoni zinazo pelekea kukatisha masomo yao, tuitumie miundombinu hii kuwapatia watoto elimu bora, kipekee niwashukuru kwa heshima kubwa mlionipa na kufikia maamuzi ya kuipa shule hii Jina langu DEUS SANGU SEKONDARI haikuwa rahisi; nitahakikisha shule hii inakuwa ni miongoni mwa shule zinazfanya vizuri kitaaluma nitahakikisha napambana na changamoto za uhaba wa waalimu na vitendea kazi kwa kupitia wadau mbalimbali na serikali ya awamu ya sita."


Aidha mbunge wa jimbo la Igalala Venant Daud Protas amesema "Maendeleo haya mnayo yaona kila mahala mhe. Rais amegusa leo ukienda kila kata ina miradi angalau 90% ya vijiji vyote kuna miradi: kwahiyo serikali hii imeamua kweli kwenda kutatua changamoto za wananchi wake."


Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Bishop Kayuni amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa Sera yake ya kujenga shule mahali pasipo na shule za sekondari lakini pia amemshuru mbunge wa jimbo hilo kwa kuchagua kata hiyo kujengwa sekondari hiyo ambayo imepewa Jina la Deus Sangu sekondari.


Kwaniaba ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya sekodari Deus Sangu Pascal Benjami Ngalu ameishukuru serikali kwa kuwaletea shule bora ambayo itapunguza mlundikano wa wanafunzi katika shule Mama ya Ilemba sekondari na kuahidi kufanya vizuri kitaaluma.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments