HOFU YATANDA KWA WAFUGAJI UGONJWA USIOFAHAMIKA KUUA NG'OMBE MANISPAA YA SHINYANGA

Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Hofu imetanda kwa wafugaji katika Manispaa ya Shinyanga baada ya ugonjwa usiofahamika kuibuka kwenye baadhi ya maeneo hususani kata ya Mwamalili na kuua mifugo hasa ng'ombe ambao wamekuwa  wakidaiwa kusumbuliwa na mapafu na kusababisha kushindwa kula majani na kusababisha vifo.


Wakizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kilichofanyika Mei 4,2023 baadhi ya madiwani wameishauri serikali kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini ugonjwa huo ambao unasababisha mifugo kuumwa mapafu kabla ya kutokea athari kubwa kwa wafugaji.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura amesema ofisi yake imepokea taarifa za mifugo kufa katika kata ya Mwamalili na inazifanyia kazi haraka iwezekanavyo na majibu yatapatikana haraka kwani mwananchi ni haki yake kuhudumiwa kwa viwango vinavyokidhi.


Aidha amewaomba Madiwani pindi panapotokea matatizo yanayoathiri wananchi kwenye maeneo yao, wasisubiri vikao vya Baraza la Madiwani bali wawasiliane na ofisi ya Mkurugenzi ili kutatua changamoto hizo haraka.

Baadhi ya wafugaji wamesema changamoto ya mifugo yao kufa ni kubwa  hivyo wameiomba serikali kuchukua hatua haraka ili kuwasaidia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments