TAASISI YA HOLLYSMILE, WASHINDI WA TUZO MDAU SHUPAVU WATOA ZAWADI KWA WAGONJWA HOSPITALI YA MKOA SHINYANGA

Taasisi ya Hollysmile, washindi wa Tuzo Mdau shupavu na wadau wa maendeleo wakiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga wakitoa zawadi kwa wagonjwa na akina Mama ambao wamejifungua watoto.

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

TAASISI ya HollySmile wakiambana na Washindi wa Tuzo ya Mdau Shupavu na wadau wa maendeleo,wametembelea Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga, na kutoa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa pamoja na akina Mama ambao wamejifungua watoto.

Ziara hiyo imefanyika leo Mei 5, 2023 ikiwa ni sehemu ya kusherehekea ushindi wa Tuzo za Mdau Shupavu 2022/2023 ambazo zimetolewa na Taasisi ya HollySmile.

Mkurugenzi wa Taasisi ya HolySmile Anold Bweichum, akizungumza Hospitalini hapo, amesema katika sherehe hizo za Tuzo za Mdau Shupavu, wameona ni vyema pia wakarudisha fadhira kwa jamii na kusaidia watu wenye uhitaji mbalimbali.

“Tumeanza kutoa zawadi ya vitu mbalimbali ikiwamo chakula, katika Kituo cha kulea watoto wenye ulemavu cha Buhangija, na sasa tupo hapa Hospitali ya Rufani mkoani Shinyanga kwa ajili ya kutoa zawadi kwa wagonjwa na kuwafariji,”amesema Bweichum.

Naye Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali hiyo ya Mkoa wa Shinyanga Selina Mpemba, amesema kitendo walichokifanya wadau hao wa maendeleo cha kutembelea wagonjwa na kuwafariji ni jambo jema na amewashukuru kwa wema walio uonyesha.

Nao wagonjwa waliopewa zawadi hizo ikiwamo Sabuni, mafuta, Pampasi za watoto, Sukari, dawa za Mswaki wameshukuru kwamba zitawasaidia katika mahitaji yao mbalimbali.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Hollysmile Anold Bweichum (kushoto) akikabidhi Zawadi Muuguzi katika Wodi ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga Esperansia Misalaba.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Hollysmile Anold Bweichum (kushoto) akikabidhi zawadi kwa Mama ambaye amejifungua katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.
Zoezi za utoaji zawadi likiendelea katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.

MC Lidya akiwa amebeba mtoto na kumpongeza Mama ambaye amejifungua katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga, ambapo leo ni siku yake pia ya kuzaliwa.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Hollysmile Anold Bweichum, akiwa ameambatana na washindi wa Tuzo ya Mdau shupavu na wadau wa maendeleo wakiwasili katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga kutoa zawadi kwa wagonjwa pamoja na kuwafariji.

Wadau wa maendeleo wakiwasili katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga kutoa zawadi kwa wagonjwa na kuwafariji.

Picha ya pamoja ikipigwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments