BENKI YA NMB KANDA YA KASKAZINI YAWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA MKOANI TANGA

 Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Praygod Godwin akizungumza na wafanyabiashara mkoani Tanga jana kuhusu namna walivyojipanga kuendelea kutoa huduma nzuri kwa wafanyabiashara pamoja na ,kuwaelezea fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye benki hiyo kushoto n i Meneja wa NMB Tawi la Madaraka Elizaberth ChawingaMeneja wa NMB Tawi la Madaraka Elizaberth Chawinga akizungumza wakati wa Halfa hiyo

Meneja wa NMB Tawi la Madaraka Elizaberth Chawinga akizungumza wakati wa Halfa hiyo


Meneja Mwandamizi wa Mikopo wa Benki ya NMB Makao Makuu Mashaga Changarawe akizungumza wakati wa kikao hicho


Meneja Mwandamizi wa Mikopo wa Benki ya NMB Makao Makuu Mashaga Changarawe akizungumza wakati wa kikao hicho


Meneja Mwandamizi wa Mikopo wa Benki ya NMB Makao Makuu Mashaga Changarawe akizungumza wakati wa kikao hicho

Sehemu ya Washiriki wa Kikao wakifuatilia kikao hicho

Na Oscar Assenga,Tanga

BENKI ya NMB Kanda ya Kaskazini leo wamefanya kikao na wafanyabiashara mkoani Tanga (NMB Business Club) huku wakieleza kwamba wamekuwa wakitoa zaidi ya Bilioni 60 kila mwezi kwa ajili ya wajasiriamali wadogo wadogo hapa nchini

Hatua hiyo inatajwa kama juhudi za benki hiyo kuunga mkono Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu kuwawezesha wajasiriamali wadogo wasogo ili waweze kujikwamua kiuchumi na hivyo kuchochea kasi ya ukuaji maendeleo.

Akizungumza wakati wa kikao hicho na wafanyabiashara ambao wanawahuduma na Meneja Mwandamizi wa Mikopo wa Benki ya NMB Makao Makuu Mashaga Changarawe ambapo alisema kwamba walianza kutoa mikopo hiyo kwa wajasiriamali tokea mwaka 2000.

Mashaga alisema kwamba hatua hiyo imewajengea uzoefu mkubwa namna ya kuwahudumia wajasiriamali hao na kwamba kutokana na utoaji wa mikopo hiyo umewawezesha kuongeza nguvu kwenye mitaji yao na hivyo kuweza kujikwamua kiuchumi.

“Leo hapa Tanga tulikutana na wateja kuwaambia kitu gani wamekianzisha na wakifanye ili kuweza kuboresha huduma zao kwa sasa wana huduma waliyoanzisha kwa ajili ya wateja wanaofanya huduma kwenye masoko yanayosimamiwa vizuri na serikali yana vizimba na wateja wameandikishwa”Alisema

Alisema kwamba ili kuhakikisha nao wananufaika na mikopo hiyo wameanza kutoa mikopo kuanzia 100,000 mpaka 1000000 bila dhamana na baadae milioni 1 hadi 2 mteja anaweka dhamana na wana mikopo mengine zaidi ya hapo inakwenda mpaka Milioni 5 kwa wateja wao.

“Lakini pia tumeanzisha mikopo kwa ajili ya vijana wanaojihusisha na bodaboda ambapo kitu ambacho kinahitajika ni kujiandikisha kwenye vyama vyao ambavyo vinatambulika na serikali na yeye ni kutafuta asilimia 20 ya chombo anachokitaka akishapata benki inaongzekja kiasi kilichobaki ili kumpatia”Alisema Meneja huyo Mwandamizi wa mikopo NMB Makao Makuu.

Hata hivyo alisema kwamba baadae wanafanya biashara na kufanya marejesho kila wiki kumaliza deni kwa kipindi cha miezi sita hadi 12 mpaka watakapoikamilisha ili kuwezesha na wengine kunufaina nayo.

Awali akizungumza Kaimu Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Benki ya NMB-Playgod Godwin alisema kwamba leo wamekutana na wafanyabiashara kuweza kutengeneza mtandao na kubadilishana uzoefu ikiwemo kuwapa mafunzo ya vitu mbalimbali na mwaka huu wamewafundisha vitu vitatu.

Alisema kikao hicho kilikuwa ni mahususi kuwakutanisha wafanyabiashara (Bussness Club) kuwakutanisha ili kuwaeleza kwamba mteja anatakiwa kuaangalia mfano anafanyabiashara ya usafirishaji anatumia petrol lakini dunia inabadilika magari mengi yanabadilika kwenye matumizi ya gesi na mama lishe anatumia mkaa lakini dunia ya leo wanatoka kwenye mkaa kwenda kwente gesi hivyo watawafundisha mbinu mbalimbali na mambo ya kurekodi taarifa za mapato na matumizi na umuhimu wake na wapo wataalamu wazuri.

Hata hivyo alisema pia wataalamu hao watawafundisha jinsi mfanyabiashara kuangaa ikitokea amepata changamoto za kiafya,uzee nani atasimamia biashara zake pia wataangalia namna ya kuwafudnisha katika mambo hayo muhimu.

Katika kikao hicho kiliwakutanisha wafanyabiashara 150 wa mkoa wa Tanga wenye matawi 12 kwa mkoa ambapo inaelezwa kwamba kitakuwa na tija kwa siku zijazo katika kuendeleza biashara zao na hatimaye kukuza mtaji wao.

Naye kwa upande wake Mfanyabiashara wa Hotel Celina Ndumbaro alisema kwamba alichojifunza katika mafunzo hayo yamewajengea uwezo wa kuweza kuona namna ya kufanya biashara zao kwa tija na kuweza kupata mafanikio.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post