ATE YAZINDUA MCHAKATO WA TUZO YA MWAJIRI BORA WA MWAKA 2023


Mkurugenzi Mkuu wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) Bi.Suzanne Ndomba akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa rasmi mchakato wa kutafuta Mwajiri bora wa Mwaka kwa mwaka 2023 uliofanyika leo Mei 30,2023 katika Ofisi za ATE Jijini Dar es Salaam

*****************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka imeendelea kuwa tukio muhimu linalotambulika katika ngazi ya kitaifa ambapo kwa miaka kadhaa sasa tuzo hizi zimehamasisha Waajiri kuweka sera bora za ajira na usimamizi wa rasilimali watu.

Pia tuzo hizi zimeweza kuchochea na kuongeza tija, mahusiano bora Mahala pa kazi, utii wa sheria na ushindani kibiashara.

Ameyasema hayo leo Mei 30,2023 Mkurugenzi Mkuu wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) Bi.Suzanne Ndomba wakati wa uzinduzi wa rasmi mchakato wa kutafuta Mwajiri bora wa Mwaka kwa mwaka 2023 uliofanyika katika Ofisi za ATE Jijini Dar es Salaam

Aidha amewaomba Waajiri wote wajitokeze kwa wingi kushiriki katika mchakato huu muhimu wa kumtafuta Mwajiri Bora wa Mwaka ambaye atatangazwa rasmi katika tukio kubwa la utoaji wa Tuzo hizi ambalo litafanyika mapema mwezi Disemba mwaka huu.

Bi.Suzanne amewahimiza kwa kuwasihi Wanachama kutembelea tovuti ya tuzo ya Mwaajiri Bora ambayo ni www.eya2023.co.tz itakayowaongoza mpaka kwenye dodoso lililoko mtandaoni.

"Makampuni shiriki yanaombwa kuwasilisha madodoso mawili yaliyojazwa, moja likiwa limejazwa na Uongozi au Mkurugenzi Mkuu au Mkuu wa kitengo cha usimamizi wa Rasilimali Watu na dodoso jingine lililojazwa na Mwajiriwa wa kawaida au Mwakilishi wa Chama cha Wafanyakazi". Amesema
Mkurugenzi Mkuu wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) Bi.Suzanne Ndomba akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa rasmi mchakato wa kutafuta Mwajiri bora wa Mwaka kwa mwaka 2023 uliofanyika leo Mei 30,2023 katika Ofisi za ATE Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) Bi.Suzanne Ndomba akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa rasmi mchakato wa kutafuta Mwajiri bora wa Mwaka kwa mwaka 2023 uliofanyika leo Mei 30,2023 katika Ofisi za ATE Jijini Dar es Salaam


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post