RAIS SAMIA ATEUA MAJAJI SITA WA MAHAKAMA YA RUFAA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewateua Majaji sita wa Mahakama ya Rufaa.


Amemteua Jaji Zainab Goronya Muruke kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Kabla ya uteuzi huo, Jaji Muruke alikuwa Jaji Mfawidhi, Kituo Jumuishi cha Mashauri ya Ndoa, Talaka na Mirathi - Temeke, Dar es Salaam

Amemteua Jaji Dkt. Benhajj Shaaban Masoud kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Masoud alikuwa Mkuu wa Shule ya Sheria Tanzania

Amemteua Jaji Amour Said Khamis kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Khamis alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora;

Amemteua Jaji Leila Edith Mgonya kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mgonya alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Masijala Kuu Dar es Salaam

Amemteua Jaji Gerson John Mdemu kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mdemu alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma

Amemteua Jaji Agnes Zephania Mgeyekwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mgeyekwa alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi

Taarifa ya Ikulu imeeleza kuwa Uteuzi huo wa Majaji wa Mahakama ya Rufani umeanza tarehe 28 Aprili, 2023 na wataapishwa kwa tarehe itakayopangwa baadae.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post