BIBI AUAWA KWA KUZIBWA PUA TUHUMA ZA KUROGA NA KUGEUZA MSUKULEBundala Rajabu mwenye umri wa miaka 32 mkazi wa Kijiji cha Ndami wilayani Kwimba mkoani Mwanza anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma za kumuua kwa kumziba pua na kumkaba kooni bibi wa miaka 87 anayeitwa Mariam Nyanda kwa imani za kishirikina.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema tukio hilo limetokea tarehe 11 ya mwezi huu ambapo inadaiwa Bundala Rajabu alikuwa anatoka kwenye shughuli zake ndipo akakutana na mtoto wake aliyefariki mwaka jana na kuzikwa katika Kijiji hicho ambapo mtoto huyo alimwambia kuwa anaishi kwa bibi Bundala

Aidha kamanda Mutafungwa amesema wakati anaongozana na mwanae huyo kwnda kwa bibi Bundala ghafla mtoto huyo alipotea katika mazingira ya kutatanisha ndipo baba huyo alipatwa na hasira na Kwenda kwa bibi huyo kumhoji wakati anamhoji ndipo akamkaba kooni na kumziba pua hali liyopelekea bibi huyokupoteza Maisha

‘Huyu mtuhumiwa baada ya kufanya tukio hilo la kikatili kabisa akiwa na Imani kwamba mtoto wake alikuwa amechukuliwa msukule na yule bibi aliondoka na kuripoti kwa jirani yake na kumwambia kuwa yule bibi aliyekuwa anatusumbua hapa kijijini na alimchukua mtoto wangu msukule sasa leo nimefunga kazi yule mwananchi akatoa taarifa kwa viongozi wa sungusungu na wakatoa taarifa polisi huyo mtuhumiwa akakamatwa.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post