WAZIRI GWAJIMA : ASILIMIA 60 YA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA HUTOKEA NDANI YA NYUMBA ZAO


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wananchi wa mkoa wa Dodoma katika maadhimisho ya Siku ya Kimataiafa ya familia,yaliyofanyika leo Mei 15, 2023 katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mwanaidi Ali Khamis akizungumza wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya familia jijini Dodoma, Mei 15, 2023.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Fatma Toufiq akieleza jambo katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya familia, jijini Dodoma Mei 15, 2023
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu akieleza lengo la maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Familia, wakati wa kongamano maalum lililofanyika jijini Dodoma Mei 15, 2023.
Mwakilishi wa mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Mrakibu msaidizi wa Polisi Dk. Ezekieli Kyogo,akizungumza wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya familia jijini Dodoma, Mei 15, 2023.
Mbunge Prof. Palamagamba Kabudi, akitoa mada katika maadhimisho hayo
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akitoa salaam za mkoa wakati wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Familia Mei 15, 2023 jijini Dodoma.
Wananchi waliojitokeza kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Familia wakifuatilia matukio mbalimbali katika maahimisho hayo jijini Dodoma, Mei 15, 2023
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akitembelea baadhi ya mabanda ya wajasiriamali na watoa huduma alipowasili katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Familia yaliyofanyika leo Mei 15, 2023.

Na Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dk. Dorothy Gwajima amewataka wazazi kujenga tabia ya kuwalinda watoto wa dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo kwa asilimia 60 vinatokea ndani ya nyumba zao.

Waziri Dk. Gwajima, ameyasema hayo leo Mei 15,2023 wakati wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya familia iliyofanyika kwenye viwanja vya Nyerere squre jijini hapa.

Dkt.Gwajima amesema kuwa wazazi wanaowajibu huo kutokana na vitendo hivyo kwa asilimia kubwa kutokea ndani ya nyumba zao na kufanya na watu wa karibu wa familia.

“Wazazi lazima tubadilike ili kulinda watoto wetu kuliko tunavyolinda mali zetu leo hii wazazi wamekuwa wepesi sana kulinda nyumba, shamba unakuta mbuzi akiibiwa tuu kwa mjumbe hakukaliki lakini watoto wetu hatuwalindi matokeo yake unakuta mtoto kafanyiwa vitendo vya ulawiti sisi hatuna hata habari”amesema Dk. Gwajima

Dkt. Gwajima amebainisha kuwa takwimu za vitendo vya ukatili hasa kwa watoto zinaonesha asilimia 60 ukatili unafanyika nyumbani hivyo msingi wa kwanza katika kutelekeza kampeni hiyo ni kuanzia ndani ya familia.

"Bila maadili na upendo familia itakuwa ni kusanyiko la watu ambapo shetani anaweza kupitisha kusudi lake kwa urahisi badala ya kusudi la Mungu hivyo, kaeni vikao mtathmini maadili na upendo wenu, mkishindwa kupendana msipeleke athari kwa watoto mje ustawi wa jamii tuwape huduma” amesema Dk. Gwajima.

Aidha Waziri Gwajima amsema kuwa wamezindua Kampeni ya Kitaifa kuhakikisha maadili yanalindwa na kuendana na mila na desturi za nchi.

''Amesema jamii yenyewe inatakiwa kuwajibika kwenye malezi yanayoendana na miiko na tamaduni za kitanzania ili kuimarisha familia na kuepuka mmomonyoko wa maadili.''amesema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Fatma Tofiq, amesema kuwa wamekutana katika siku hiyo ya kimataifa ya familia kujadilina nini kifanyike na kipi kisifanyike ili kuimarisha familia.

“Maadili yakiwepo katika familia zetu hakutakuwepo na watoto wa mitaani lakini pia tunapaswa kumrudia Mungu kuna mambo yanatendeka hivi sasa yanaumiza sana lakini wajibu wa kila familia kuwa na upendo na kila mtu baba au mama kuwa na wajibu wa kulinda familia yake”amefafanua

Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt.John Jingu ,amesema amadhumuni ya Siku ya Kimataifa ya familia amebainisha kwamba siku hii ni Azimio la kimataifa lililofikiwa mwaka 1993 kupitia baraza la Umoja wa Mataifa.

Dkt. Jingu ametoa wito kwa jamii kuitumia siku hii kutafakari na kuona namna gani familia zinatimiza jukumu la malezi na ustawi wake.

"Kaulimbiu ya Siku ya Kimataifa ya Familia, inatualika kuona umuhimu wa kuimarisha maadili na upendo katika familia zetu ili ziwe imara kwa manufaa ya jamii na Taifa kwa ujumla" amesema Dkt. Jingu.

Kwa upande wake Mwakilishi wa mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Mrakibu msaidizi wa Polisi Dk. Ezekieli Kyogo, amesema kuwa kama familia zitakuwa sawa mzigo wa matukio ya uharifu yatapungua nchini.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule,amepongeza juhudi za Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum kwa juhudi za kutoa za Elimu juu ya umuhimu wa Familia na Upendo katika Jamii zetu.

“Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum inafanya kazi nzuri sana kwani kauli mbiu ya “linda maadili “imesambaa sana katika jamii zetu na kumshawishi kila mmoja wetu kuwekeza katika Kulinda maadili na kupinga mmonyoko wa Maadili Nchini”RC Senyamule.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments