JUMUIYA YA WAZAZI CCM SHINYANGA MJINI WATEMBELEA MIRADI KAMBARAGE, MJINI...WASISITIZA MALEZI, ELIMU & UTUNZAJI MAZINGIRA

Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini na viongozi wa mtaa wa Miti Mirefu kata ya Mjini wakitembelea mradi wa Bustani ya kupumzikia iliyopo eneo la Mataa NBC

Na Kadama Malunde- Malunde 1 blog
Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini imefanya ziara katika Kata ya Kambarage na Mjini kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wanachama na viongozi wa CCM.

Ziara hiyo ambayo ni mwendelezo wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja/Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini kutembelea kata zote 17 za wilaya hiyo imefanyika leo Jumatano Mei 17,2023.

Miongoni mwa miradi iliyotembelewa ni pamoja na mradi wa Bustani ya kupumzikia eneo la Mataa NBC Mjini Shinyanga na ujenzi wa madarasa mawili na matundu matatu ya vyoo katika shule ya awali na msingi Mwenge utakaogharimu sh. Milioni 58 unaotarajiwa kukamilika ifikapo Juni 15,2023 na ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na ofisi moja katika shule ya awali na msingi Jomu utakaogharimu sh. milioni 100 ukitarajiwa kukamilika tarehe 30.6.2023.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhe. Fue Mrindoko ameupongeza uongozi wa Kata ya Mjini na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa ubunifu wa kuanzisha mradi wa Bustani ya kupumzikia ili kuboresha mandhari ya Mji wa Shinyanga.

Kuhusu ujenzi wa vyumba vya madarasa Mrindoko amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili utekelezaji wa miradi ya maendeleo hivyo kuwaomba wananchi kutunza miradi na kuendelea kumuunga mkono katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini wakishiriki ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Mwenge

Mrindoko pia amesisitiza umuhimu wa jumuiya za CCM kuanzisha miradi ya maendeleo akisisiza kuwa kwa upande wao hivi karibuni wataanzisha mradi wa kufyatua matofali.

Aidha amewaomba wanaCCM kusimama imara kwenye uchaguzi ujao wa serikali za mitaa kwa kuhakikisha wanaweka viongozi wenye uwezo wa kazi na wanaokubalika ili CCM iendelee kushika dola huku akihamasisha ushirikiano na mshikamano ndani ya CCM.

Kwa upande wake, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Yotham Kibabi amewasisitiza wananchi kupeleka watoto shule na kutunza mazingira kwa kupanda miti kwa ajili ya manufaa ya kizazi kilichopo na kijacho huku akihamasisha kila mmoja kutimiza wajibu wake katika malezi ya watoto.

“Ni jukumu la kila mmoja kusimamia suala la maadili ili kutokomeza vitendo viovu ikiwemo ushoga na usagaji. Sisi Umoja wa wazazi tumepewa jukumu la kusimamia elimu, malezi na mazingira hivyo ni lazima tuyasimamie haya. Nasisitiza pia jamii kuachana na vitendo vya ukatili wa kijinsia”,amesema.

“Watoto wetu wetu wanafanyiwa ukatili na ndugu wa karibu, tuache tabia ya kuwalaza chumba kimoja na wageni na tuwe makini na watu wetu wa karibu. Kuna mababu wengine ni vimbulu kabisa, wanawafanyia ukatili watoto kwa kuwabaka na kuwalawiti. Kuna wababa wengine wanatembea na wasichana wa kazi hii ni tabia mbaya, Mtoto wa mwenzako ni wako,mlinde”, amesema Kibabi.

Aidha ametumia fursa hiyo kuwasisitiza wazazi na walezi kupeleka watoto shule huku akiwataka wanandoa kufanya kazi za kuwaingiza kipato kwa ajili ya ustawi wa familia yao.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini na viongozi wa mtaa wa Miti Mirefu kata ya Mjini wakitembelea mradi wa Bustani ya kupumzikia iliyopo eneo la Mataa NBC leo Jumatano Mei 17,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza kwenye mradi wa Bustani ya kupumzikia iliyopo eneo la Mataa NBC kata ya Mjini 
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini na viongozi wa mtaa wa Miti Mirefu kata ya Mjini wakipiga picha ya kumbukumbu kwenye mradi wa Bustani ya kupumzikia iliyopo eneo la Mataa NBC
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Yotham Kibabi akiwa amekaa kwenye Bustani ya kupumzikia iliyopo eneo la Mataa NBC
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Michael Kema akisoma taarifa ya ujenzi wa madarasa mawili na matundu matatu ya vyoo katika shule ya awali na msingi Mwenge
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini wakishiriki ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Mwenge
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini wakishiriki ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Mwenge
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini wakiwa kwenye mradi wa ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Mwenge
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Yotham Kibabi akizungumza kwenye mradi wa ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Mwenge
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza kwenye mradi wa ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Mwenge
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza kwenye mradi wa ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Mwenge
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Yotham Kibabi akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Mjini
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Mjini
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akiwatambulisha Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya hiyo.

Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Esther Makune akizungumza
Kiongozi CCM Kata ya Mjini, Seleman Magubika akisoma taarifa ya utekelezaji ya kata ya Mjini

Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Samwel Jackson akizungumza kwenye kikao 
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji wilaya ya Shinyanga Mjini Daniel Kapaya akizungumza kwenye kikao
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji wilaya ya Shinyanga Mjini Giti Boniphace akizungumza
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji wilaya ya Shinyanga Mjini Zulfa Hassan akizungumza
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji wilaya ya Shinyanga Mjini, Mary Makamba akizungumza
Mjumbe wa Kamati  ya Utekelezaji Wilaya ya Shinyanga mjini, Hasna Maige akizungumza kwenye kikao
Mjumbe wa Kamati  ya Utekelezaji Wilaya ya Shinyanga mjini akizungumza
Katibu wa Elimu, Malezi na Mazingira CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Richard Mseti akizungumza kwenye kikao

Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko (kulia) akimkabidhi mmoja wa wananchi kadi ya CCM

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza katika shule ya awali na msingi Jomu kata ya Kambarage
Mwalimu Mkuu wa shule ya awali na msingi Jomu, Pendo Peter Himbi  akisoma taarifa ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na ofisi moja
Kikao kikiendelea katika shule ya awali na Msingi Jomu kata ya Kambarage
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko na viongozi mbalimbali wakiwa katika shule ya awali na msingi Jomu kata ya Kambarage
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko, Wajumbe wa kamati ya utekelezaji na viongozi mbalimbali wakiangalia ujenzi wa madarasa katika shule ya awali na msingi Jomu kata ya Kambarage

Katibu wa CCM kata ya Kambarage, Khamis Haji akizungumza wakati wa kikao cha wanachama na viongozi wa CCM
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji Leonard Mapolu akisoma taarifa ya utekelezaji kata ya Kambarage
Diwani wa kata ya Kambarage Hassan Mwendapole akizungumza wakati wa kikao cha wanachama na viongozi wa CCM
Diwani wa Viti Maalum Mhe. Shella Mshandete akizungumza wakati wa kikao cha wanachama na viongozi wa CCM
Mwenyekiti wa Wazee Wilaya ya Shinyanga Benard Itendele akizungumza wakati wa kikao cha wanachama na viongozi wa CCM
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kambarage Mchungaji Amos Maday akizungumza wakati wa kikao cha wanachama na viongozi wa CCM
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Yotham Kibabi akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Kambarage
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Yotham Kibabi akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Kambarage
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Kambarage

Wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Kambarage wakiwa kwenye kikao
Wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Kambarage wakiwa kwenye kikao.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post