MBUNGE AHMED : TANZANIA NI MIONGONI MWA NCHI CHACHE DUNIANI TUNAISHI KWA RAHA

“Tanzania ni miongoni mwa nchi chache Afrika na duniani ambazo mpaka sasa hivi Ina amani na tunaishi kwa raha, iwe ni wafanyabiashara, wafanyakazi na Watanzania ambapo Moja ya sababu kubwa ni uwepo wa jeshi letu ambalo wanafanya kazi usiku na mchana”, Mhe. Ahmed.

Ni Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Salum wakati akichangia bajeti ya Wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga Taifa hotuba iliyowasilishwa na Waziri wa wizara hiyo Mhe. Innocent Bashungwa Leo Mei 24, 2023 bungeni jijini Dodoma.
Ametoa pongezi kwa majeshi yote hapa nchini kwa kujitoa kwao muhanga na kutoa maisha yao kwaajili ya kulinda amani ya nchi huku akitoa ushauri kwa serikali kuweka mipango mikakati ya kuboresha majeshi kuwa ya kisasa zaidi.


“Mliwahi kusikia huko Kusini Kuna wakati ilitokea taharuki ya hapa na pale kazi kubwa ilifanywa na jeshi letu la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kuna vijana kule wamekaa kwenye mapori mazito ambao wako tayari kujitoa mhanga na kutoa maisha yao kwa ajili ya Muungano wa Tanzania”, amesema Mhe. Ahmed

“Upo umuhimu wa kuweka mpango wa kuboresha jeshi la Tanzania kutoka hapa tulipo na kuwa katika Moja ya jeshi Bora Afrika kwa kubadilisha mitambo, kuboresha mawasiliano na jeshi likawa la kisasa zaidi”,amesema Mhe. Ahmed.


Hata hivyo amehitimisha kwa kuunga mkono kipengele cha kushirikisha sekta binafsi katika kuliendeleza jeshi.


“Tutaingia partner ship na sekta binafsi katika kuliendeleza jeshi, wapo wenye uwezo mkubwa sana, mainjinia wazuri hivyo ni swala la kukaa na kuwa na mipango Ili kama zimekuja sekta binafsi waziri leta tuzupitishe hapa bungeni”. ameongeza Mhe. Ahmed

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments