TANESCO SHINYANGA YATOA TAHADHARI WIMBI LA WIZI WA VIFAA KINGA KWENYE TRANSFOMA, MIUNDOMBINU YA UMEME

TAARIFA YA WIZI WA VIFAA KINGA KWENYE TRANSFOMA NA KWENYE MIUNDOMBINU YA UMEME ILIYOPO MKOA WA SHINYANGA

Habari ndugu wateja, kumeibuka wimbi la wizi wa vifaa kinga kwenye miundombinu yetu ya umeme ikiwemo transfoma (copper wire zinazolinda miundombinu ya umeme dhidi ya radi, stay wire zinazoshikilia nguzo zisianguke) vilivyopo maeneo mbalimbali katika mkoa wetu na kupelekea ukosekanaji wa umeme kwa wateja wa maeneo hayo.

Yafuatayo ni baadhi ya maeneo ambayo vifaa kinga hivyo vimekuwa vikiibiwa mara kwa mara :-

Numbiri, Ibadakuli - jirani na Istquama, Kitangiri round bar, Ibinzamata, Ilwelyangula na mto Mhumbu.

Shirika linatoa tahadhari kwa wananchi wote kutokujihusisha na vitendo hivyo kwani vinasababisha kukatika kwa umeme mara kwa mara na kulisababishia shirika ukosefu wa mapato.


Tunaomba tushirikiane kulinda miundombinu na kupewa taarifa haraka pindi unapotilia shaka utendaji kazi wa baadhi ya watu kwenye miundombinu ya umeme.


TANESCO - SHINYANGA
14.04.2023

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments