WAZIRI AWESO ATOA AGIZO KWA MKURUGENZI WA MAMLAKA ZA MAJI NCHINI



Waziri wa Maji Jumaa Aweso akisisitiza jambo kwa Mkuu wa wilaya ya Korogwe Jokate Mwogelo leo wakati wa ziara yake katika Mji wa Korogwe ambaye ilikuwa na lengo la kuangalia tatizo la upatikanaji wa maji katika mji huo

Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza leo wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani Korogwe

Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji Mji Korogwe Mhandisi Sifael Masawa akieleza jambo wakati wa ziara hiyo


MKUU wa wilaya ya Korogwe Joketi Mwogelo akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto ni Waziri wa Maji Jumaa Aweso

Waziri wa Maji Jumaa Aweso kushoto akimsikiliza kwa umakini Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Timotheo Mzava wakati wa ziara hiyo anayewafuatia kwa nyumba ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM)

Waziri wa Maji Jumaa Aweso katikati akiwa na Mkuu wa wilaya ya Korogwe Joketi Mwogelo kushoto wakati wa ziara yake wilayani Korogwe


Na Oscar Assenga, KOROGWE

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amemuagiza Mkurugenzi wa Idara ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira ,Wizara ya Maji CPA Joyce Msiru kuziangalia Mamlaka za Maji Usafi wa Mazingira katika Miji mbalimbali nchini ili wakurugenzi wao waendane na mazingira ya elimu yao kuliko ilivyo sasa.

Sambamba na hilo akaagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Maji wa Korogwe mjini Mhandisi wa Maji Korogwe Mji Sifael Masawa kupangiwa kazi nyengine kutokana na kushindwa kutatua changamoto ya maji kwenye kwenye eneo lake

Aweso aliyasema hayo leo wakati wa ziara yake katika Mji wa Korogwe ambaye ilikuwa na lengo la kuangalia tatizo la upatikanaji wa maji katika mji huo licha ya kuwepo kwa vyanzo vya maji ikiwemo Mto Pangani ambao unapita katikati ya mji huo.

Hatua hiyo ni baada ya kufika wilayani humo na kupata taarifa kuhusu miradi ya maji inayotekeleza kwenye mji huo ambapo alionyesha kutokuridhishwa na namna mtendaji huyo anavyoshughulia jambo hilo ili liweze kupata majawapo yake.

Alisema haiwezekani mji huo kukosa huduma hiyo muhimu wakati kuna vyanzo ambavyo vinaweza kutumika kuweza kuondosha changamoto hivyo lakini kutokana na usimamizi mbovu unapelekea kuwepo wa hali hiyo na wao kama wizara hawawezi kukubali kuona jambo hilo.

“Mkurugenzi wa Idara ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira ,Wizara ya Maji CPA Joyce upo hapa naagiza Mamlaka zote hapa nchini aina ya Korogwe tuangalie wakurugenzi wao taaluma zao ziendane na mazingira yao sambamba na elimu mimi sitamtoa kwenye kazi lakini huyo wa hapa Mkurugenzi wa Maji Korogwe Mji Mhandisi Sifale Masawa ni mzuri lakini apelekwe sehemu ambayo inaendana na mazin gira yta elimu yake”Alisema Waziri Aweso.

“Umeshakuwa Mkurugenzi hapa jiendeleze kielimu…fursa zipo nyingi za vyuo hatuwezi kwenda hivi lakini Katibu Mkuu wa Wizara leo mkae mpange mje muona namna ya kufanya hapa Korogwe kama ni suala la kutoa miundombinu ya zamani tuona tunafanyaje”Alisema

“Lakini sio tunakaa na kulalamika wakati mto Pangani upo hapa tunaendelea kuteseka lakini hitaji hilo liendane na miji ya 28 na fedha za awali zimeshatolewa”Alisema

Katika hatua nyengine,Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameagiza kupelekwa Mkurugenzi mwengine Korogwe na yeye kupangiwa sehemu nyengine ufanye kazi ambayo itaendana na mazingira ya hapa kwenye mji wa Korogwe kutokana na kwamba wanahitaji kusaidiwa hivyo hapoa wataona namna ya kumuweka mtu mwengine .

“Hapa tutamuweka mtu mwengine atusaidie kwani hata mazingira haya ushindwe hata ofisi kuboresha ndio maana hata huna kujiamini lakini ninachojua mtaalamu wa maji ni mtu ambaye amesomea maji ndio mtu anasema mambo yanakuwa safi hakuna kipaumbele nini kifanyike kuondosha tatizo la maji bado umeendelea kukaa kimya bila kupatikana kwa suluhu”Alisema Aweso

Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji Mji Korogwe Mhandisi Sifael Masawa alisema kuwa mamlaka hiyo imakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa miundombinu ya maji hali ambayo inasababisha kuwepo na uhaba wa maji.

Alisema kuwa licha ya kuwa na vyanzo vingi vya maji hali ya upatikanji wa maji kwa sasa ipo katika asilimia 70 lakini changamoto ya uhaba wa umeme mdogo pamoja na kutokuwewepo na mtambo wa kusafisha maji kumesababisha uwepo wa changamoto hiyo.

“licha ya jitihada za serikali kutuletea mitambo kwa ajili ya uchimbaji wa visima saba tunauhitaji wa fedha takribani sh Mil 825 kwa ajili ya uwekaji wa miundombinu ya usambazaji wa maji baada ya maji kupatikana .





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post