WALIOPANDIKIZWA FIGO MLOGANZILA WARUHUSIWA, WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUWAREJESHEA TABASAMU

Naibu Mkurugenzi Mtendaji MNH-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi akizungumza na waandishi wa habari akielezea mafanikio makubwa yaliyopatikana Mloganzila katika kipindi cha awamu ya sita ikiwemo upandikizaji wa figo.
Daktari Bingwa wa Upasuaji Mishipa ya Damu na Upandikizaji Viuongo kutoka Korea Kusini Prof. Park Kwan Tae akielezea namna ushirikiano uliopo baina ya KOFIH na Mloganzila ulivyosaidia katika uboreshaji wa huduma za afya.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila akielezea sababu pamoja na dalili za ugonjwa wafigo.

Daktari Bingwa wa Upasuaji Mfumo wa Mkojo na Figo akizungumza na waandishi wa habari.
Baadhi ya wagonjwa waliopandikiziwa figo wakiwa katika picha ya pamoja na wataalamu walioshiki katika zoezi hilo.
Baadhi ya wataalamu walioshiriki zoezi wakiwa katika hafla ya kuwaaga wagonjwa hao.
Baadhi ya wagonjwa waliopandikiziwa figo wakiwa katika picha ya pamoja na wataalamu walioshiki katika zoezi hilo.
Baadhi ya wagonjwa waliopandikiziwa figo wakiwa katika picha ya pamoja na wataalamu walioshiki katika zoezi hilo.


********************


Watu watatu waliopandikizwa Figo Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila na watatu waliowachangia Figo wameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya afya zao kuimarika ambapo wametoa shukrani kwa Rais Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Uongozi wa Mloganzila.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Bi, Masungwa Mangu amesema matumaini yake yamerejea baada ya kupandikizwa Figo kwa kuwa alipata changamoto cha Figo toka mwaka 2016 na mwaka 2020 alianza matibabu ya kuchuja damu (Dialyisis).


"Nafurahi kuwa mtanzania wa kwanza kupandikizwa Figo Mloganzila, nimepata huduma nzuri sana hapa. Toka nimeanza kuumwa nimepitia changamoto nyingi ikiwemo gharama kubwa ya kuchuja damu, nawashukuru wanafunzi wenzangu wa Chuo cha Ushirika Moshi kwa kunichangia fedha za matibabu, namshukuru kaka yangu ambaye amejitolea kunichangia Figo kwa sasa naendelea vizuri nimeruhusiwa kurudi nyumbani" ameeleza Bi Masugwa


Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mtendaji MNH-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi amesema kuwa mbali na Mloganzila kuwa hospitali ya tatu kupandikiza figo nchini lakini imeweka rekodi ya kuwa hospitali ya kwanza kutoa figo kutoka kwa wachangiaji kwa kutumia matundu madogo (Hand Assisted Laparoscopic Nephrectomy) ambao haujawahi kufanyika popote hapa Tanzania na Afrika mashariki na kati.


“Kwa kuanzia Mloganzila imeshirikiana na mtaalamu mwelekezi kutoka Korea Kusini Prof. Park Kwan Tae ambaye amewafanyia mafunzo wataalamu wazawa katika eneo la upasuaji na upandikizaji figo, na wataalamu wa MNH-Upanga ambao tayari wamebobea katika kupandikiza figo.Siku za usoni tunategemea wataalamu wazawa wataweza kufanya upandikizaji figo wenyewe bila kuhitaji uangalizi ameeleza Dkt. Magandi


Naye mshauri mwelekezi kutoka nchini Korea Kusini Dkt. Park Kwan Tae amesema kuwa amefurahi kufanya kazi na wataalamu wa Mloganzila na kwamba yupo tayari kuendeleza ushirikiano katika kuanzisha huduma za kibingwa


Kuanza kwa huduma za upandikizaji figo Mloganzila ni mwendelezo wa kutekeleza mkakati wa Serikali wa kuhakikisha kuwa huduma za kibingwa zinapatikana nchini.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post