WAFANYAKAZI OFISI YA WAZIRI MKUU WAHIMIZWA KUTUNZA SIRI ZA OFISI


Na: Mwandishi wetu-DODOMA

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Leonard Mchau amewahimiza wafanyakazi wa ofisi hiyo kufanya kazi kwa weledi na kutunza siri za ofisi.

Kauli hiyo ameitoa Aprili 28, 2023 wakati akifungua mafunzo ya siri na utunzaji wa nyaraka kwa Makatibu Mahususi na Wasaidizi wa kumbukumbu yaliyofanyika Jijini Dodoma.

Amesema kutokana na kukua kwa sayansi, teknolojia na mawasiliano kunachangia kuvuja kwa siri za ofisi kutokana na baadhi ya wafanyakazi kutumia vibaya teknolojia na kufanya kazi kwa mazoea bila kuzingatia miongozo iliyowekwa na serikali katika kutoa taarifa za ofisi.

“Fanya kazi kwa tija acheni kufanya kazi kwa mazoea na timizeni majukumu yenu kwa wakati” amesema.

Aidha, Mchau amewahimiza wafanyakazi hao kutojihusisha na vitendo vya rushwa vinavyoweza kuvujisha nyaraka za siri.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post