TGNP YATOA MAPENDEKEZO JUU YA BAJETI KWA WIZARA

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Lilian Liundi akizungumza leo Aprili 11,2023 Jijini Dar es Salaam na wadau mbalimbali na kujadili kuhusu mlango wa kijinsia katika Bunge la Bajeti linaloendelea hivi sasa.

*********

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MTANDAO wa Jinsia Tanzania TGNP umesema ni vyema bajeti za Wizara mbalimbali zinazopangwa zikafuatiliwa kwa kina katika utekelezaji wake na watu wote ili kuzuia mianya ya rasilimali za wananchi kutumika vibaya kama ambavyo ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa serikali imebainisha.

Ameyasema hayo leo Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Lilian Liundi wakati walipokutana na wadau mbalimbali kujadili kuhusu mlango wa kijinsia katika Bunge la Bajeti linaloendelea hivi sasa.

Amesema wamekuwa wakishirikiana na Wizara mbalimbali katika kutoa mafunzo kwenye kufanya uchechemuzi kwenye masuala ya bajeti yenye mlengo wa kijinsia kwenye hizo Wizara mbalimbali.

Hata hivyo amesema wamefanya uchambuzi wa kijinsia na kupitia kuangalia utekelezajikila baada ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano wanakuwa wanatoa msimamo wao kwa mlengo wa kijinsia.

Aidha ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kuonesha na kuendeleza usawa wa kijinsia katika kujenga rasilimali kwa mlengo wa kijinsia ikiwemo kuongezaka kwa upatikanaji wa maji vijijini.

"Kuongezeka kwa upatikanaji wa maji vijijini kutoka asilimia 72.3 mwaka 2021 hadi asilimia 74.5 mwaka 2022 na kwa upande wa mijini asilimia 86 mwaka 2021 hadi asilimia 86.5 mwaka 2022". Amesema

Viongozi wa kiserikali wakiwemo madiwani pamoja na wenyeviti wa mitaa wamesema viongozi haswa watendaji wanapaswa kuzingatia sheria taratibu za uongozi nchini.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post