SIMBA SC YASHINDWA KUFURUKUTA MBELE YA RAJA CASABLANCA, YANYUKWA 3-1Simba SC imemaliza michezo ya hatua ya makundi kwa kufungwa 2-1 dhidi ya kinara wa kundi hilo, Raja Casablanca (Morocco) aliyeshinda michezo 5 na kusare 1 hivyo kupata alama 16.

Raja Casablanca ilianza kupata bao kupitia kwa Hamza Khabba kabla ya Simba Sc kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wao hatari raia wa DR Congo Jean Baleke.


Mabao mengine yalifungwa na Mohamed Boulacsou pamoja na Hamza Khabba ambaye kwenye mchezo huo aliweza kupachika mabao mawili na kuisaidia timu yake kuondoka na ushindi huo mnono.


Simba SC wapili akiwa na alama 9, AC Horoya ((Guinea) wa tatu akiwa na alama 7 ilhali Vipers FC (Uganda) imeshika mkia ikiwa na alama 2.


Raja Casablanca na Simba SC walishafuzu hatua ya robo fainali hivyo wanasubiri droo ambayo iyachezeshwa Jumatano Aprili , 2023 nchini Misri

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post