MRADI WA MAJI MIJI 28 KAZI YAANZA RASMI, AWESO ATOA WITO KWA WAKANDARASI

Waziri wa maji Mhe Jumaa Aweso(MB) amekutana na kufanya mazungumzo na makampuni ya wakandarasi wanayotekeleza Mradi mkubwa wa kihistoria na wa kimkakati wa Miji 28 chini ya ufadhili wa Benki ya Exim ya India kwa lengo la kutakia kila lakheri wanapoanza rasmi utekelezaji wa miradi na kuwapatia maelekezo mahususi ya namna bora ya kutekeleza miradi hii kwa wakati na ubora unaotakiwa .

Aidha Waziri Aweso amewataka wakandarasi kufanya kazi hii kwa nguvu kubwa sana kwani wananchi wamesubiri kwa muda mrefu kuanza kwa kazi hii akisisitiza kuwa yeye binafsi atasimamia hatua zote za ujenzi na kufuatilia Utekelezaji wake kwa ukaribu sana.

Zaidi amewaeleza matarajio na matamanio ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye alishuhudia utiaji saini wa Miradi hii.

Utekelezaji rasmi umeanza tarehe 12 mwezi april 2022 baada ya serikali kukamilisha taratibu za masuala ya kodi na kulipa malipo ya awali (Advance payment) kwa wakandarasi hao na sasa rasmi wametawanyika maeneo yalio katika mpango na kazi imeanza.

Mradi huu utanufaisha miji ya kaliuwa, sikonge, urambo, kasulu, mpanda,kilwa masoko, nanyumbu, ifakara, rujewa, makambako, njombe, wangingombe, chunya,chamwino, chemba, singida, manyoni, mugumu, geita, kayanga, chato, handeni, korogwe, muheza, pangani, mafinga, songea, rorya / tarime, na makonde.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments