AJIUA CHUMBANI AKIACHA MKEKA WA MADENI ANAYODAIWAKamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Mwanaume aitwaye Ally Hamis (48) amejiua kwa kujinyonga ndani ya nyumba yake katika kijiji cha Itwangi Wilaya ya Shinyanga huku akiacha ujumbe kuhusu madeni anayodaiwa ndugu zake wayalipe.

Inaelezwa kuwa tukio hilo limebainika kutokea leo Jumamosi Aprili 8, 2023 asubuhi baada ya familia kumkuta Ally Hamis amejinyonga ndani ya nyumba yake.


Mwenyekiti wa kijiji cha Itwangi Kisendi Lubinza amesema Ally ameacha ujumbe kwa kuorodhesha madeni anayodaiwa na kuwaomba ndugu zake kulipa madeni hayo likiwemo deni la baskeli yake aliyokuwa anadaiwa sh 40,000/= , baba yake mdogo alipwe laki tatu na mwingine alipwe debe moja la mahindi.


"Kwenye ujumbe wake pia ameandika  ‘nimeamua kujiua mimi mwenyewe asishikiliwe mtu yoyote nimeamua kwa moyo wangu, nimeamua kumfuata Mama yangu aliyetangulia mbele za haki miaka mingi iliyopita", ameeleza Mwenyekiti huyo wa kijiji.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.


“Ni kweli mwanaume huyo amejinyonga na ameacha ujumbe kuwa ana madeni kwa hiyo askari wameenda kukagua eneo la tukio ambapo mwili umefanyiwa uchunguzi na daktari na ndugu  wamekabidhiwa kwa ajili ya mazishi”, amesema Kamanda Magomi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post