DC TANGA ATAKA VIONGOZI WA DINI KUENDELEA KUKEMEA NDOA ZA JINSIA MOJA

 

Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akipata futari iliyoandaliwa na Shirika la Bima la Taifa (NIC) jana nyumbani kwake eneo la Raskazone Jijini Tanga kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shillow
Shehe wa Mkoa wa Tanga Jumaa Luwuchu akipata futari iliyoandaliwa na Shirika la Bima la Taifa (NIC) iliyofanyika nyumbani kwa Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa
Wadau mbalimbali wakipata futari wa pili kulia ni Mwandishi Mwandamizi wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) Mkoa wa Tanga Bertha Mwambela akifuatiwa na Mwandishi wa Gazeti la Habari Leo Amina Omari na aliyevaa mtandio mweuzi ni Mwandishi wa Chanel Ten Mkoa wa Tanga Raya Kipingu 
Mwandishi wa Azam TV Mkoa wa Tanga Mariam Shedafa akipata futari iliyoandaliwa na Shirika l;a Bima la Taifa (NIC) nyumbani kwa Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandiliwa 
Mwandishi wa Azam TV Mkoa wa Tanga Mariam Shedafa akipata futari iliyoandaliwa na Shirika l;a Bima la Taifa (NIC) nyumbani kwa Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandiliwa 
Futari ikiendelea 
Mwandishi wa Gazeti la Habari Leo Amina Omari akipata futari 
Sehemu ya wadau wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Mkoani Tanga wakipata futari

MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa kulia akipata futari iliyoandaliwa na Shirika la Taifa la Bima (NIC) na kufanyika nyumbani kwake eneo la Raskazone Jijini Tanga kulia ni Shehe wa Mkoa wa Tanga Jumaa Luwuchu akifuatiwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shillow
Sehemu ya wadau wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) wakipata futari hiyo
Meneja wa Tanroad Mkoa wa Tanga katikati akiwa na viongozi wengine wakipata futari hiyo
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza jambo wakati wa futari hiyo
Mwakilishi wa Mkurungenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Bima nchini (NIC) Herman Mushi akizungumza wakati wa halfa hiyo

Shehe wa Mkoa wa Tanga Jumaa Luwuchu akizungumza wakati wa halfa hiyo
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shillow

Na Oscar Assenga, TANGA. 

Mkuu wa wilaya ya Tanga Mkoa wa Tanga Hashim Mgandilwa amesema viongozi wa dini wana jukumu kubwa la kuendelea kuielimisha jamii juu ya athari za matendo yasiyopendeza mwenyezi Mungu ikiwemo kukemea ndoa za jinsia moja 

Mgandilwa aliyasema hayo Aprili 13 mwaka huu wakati wa Futari iliyoandaliwa na Shirika la Bima la Taifa (NIC) na kufanyika nyumbani kwake eneo la Raskazone Jijini Tanga ambapo alisema vitendoi hivyo vinavunja mila na tamaduni za kitanzania. 

Alisema kupitia hadhara hiyo anaitumia kuendelea kukumbusha wazazi kwani wamekuwa bize na utafutaji mwisho wa siku wanashindwa kutekeleza majukumu ya kulea familia. 

“Niwaombe leo tunalalamika masuala la ushoga na usagaji hayo yote yanatoka kwenye nyumba zetu hivyo hivi sasa turudi nyumbani tujitathimini turudi kwenye malezi ya muhimu kwenye watoto wetu”Alisema 

“Hivi karibu Wizara ya Afya ilitoa waraka wa kuzuia watoto wadogo kuanza kupelekea hostel leo ilifikia kipindi mtoto akiwa na miezi mitatu au minne anaachishwa kunyonyeshwa na kupelekwa day care analelewa watoto wanapoteza mahaba na wazazi wao “Alisema 

Mkuu huyo wa wilaya aliwaomba wazazi na viongozi wa diuni watumie wasaa huo kuwakumbusha wazazi kuwaleta watoto wao kutokana na kwamba hivi sasa wamehama kwenye malezi sasa wapo kwenye kuzaa lakini hatutaki kulea wajitahidi watenge muda wakae na watoto wawajenge kama wao walivyojengwa huko nyuma. 

Amesema kuwa viongozi wa dini wanajukumu la kuendelea kielimisha waumini wao juu ya athari za matendo yasiyo mpendeza mungu katika jamii. 

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba mkoa huo nan chi kwa ujumla wapo kwenye janga la ndoa za jinsia Moja sambamba na kishamiri kwa vitendo vya ushoga. 

“Hivyo tunaomba viongozi wa dini tushirikiane katika vita hii Ili vizazi vilivyopo na vijavyo viweze kubaki salama kwa sababu vitendo hivyo havikubaliki”Amesema DC Mgandilwa. 

Awali akizungumza katika Futari hiyo Shekhe wa mkoa wa Tanga Jumaa Luwuchu amesema kuwa wao viongozi wa dini wanaendelea kukemea vikali vitendo hivyo huku akiwataka wazazi na walezi kurudi katika kulea watoto katika maadili yaliyo mazuri. 

Luwuchu alisema matokeo ya matendo hayo ni vitendo viovu vinavyotokana na wazazi kukaaa kimya wakati watoto wao walivyokuwa wameanza kuvaa nguo wakiwa wamezishusha chini ya makalio hivyo umefika wakati waimarishe malezi ya watoto katika maeneo yote. 

Naye kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurungenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Bima nchini (NIC) Herman Mushi amesema kuwa shirika hilo limepunguza madai ya malipo ya fidia na Sasa yanalipwa ndani ya siku Saba toka majanga kutokea. 

Alisema ndo maana Shiriki hilo limekuwa namba moja katika utendaji wa kazi kwenye makampuni zote za bima zilizopo hapa nchini kwa kukua na kwa kipato ,kiwango cha mali na fedha. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post