LEAT WATOA ELIMU YA MSAADA WA KISHERIA KWA WANANCHI WA MPOMVU GEITA

Timu ya Wanasheria watetezi wa Mazingira kwa vitendo LEAT wakitoa elimu ya msaada wa kisheria kwa wananchi wa Mpomvu Geita

Na Marco Maduhu, GEITA

TIMU ya Wanasheria watetezi wa Mazingira kwa vitendo (LEAT), wametoa elimu ya msaada wa kisheria kwa wananchi wa Mtaa wa Mpomvu Kata ya Mtakuja Halmashauri ya Geita Mji.

Elimu hiyo imetolewa leo Aprili 19,2023 kwenye Mkutano wa hadhara ambao umefanyika katika Soko la Mpomvu.

Mwanasheria kutoka (LEAT) Clay Mwaifani, akitoa elimu hiyo ya msaada wa kisheria kwa wananchi wa Mpomvu, amesema sheria ikifuatwa vizuri nchi hii haitakuwa na Migogoro ya ardhi wala Migogoro ya aina yoyote ile ikiwamo ya uchafuzi wa mazingira.

Clay ambaye pia ni Afisa Miradi, amesema Migogoro mingi inatokana na baadhi ya watu kupindisha Sheria, na kuwaonea wale ambao hawajui sheria na kunyimwa haki zao, hivyo wao kama Wanasheria kutoka (LEAT) wamekuwa wakitoa elimu kwa wananchi ya msaada wa kisheria, ili watambue namna ya kupata stahiki zao.

"Sheria zikifuatwa vizuri hakutakuwa na Migogoro ya Ardhi, wala Migogoro ya aina yoyote ile na chini itabaki kuwa na Amani," amesema Mwaifani.

Pia, amewataka wananchi kuitekeleza sheria ya mtoto ya mwaka 2009 kifungu cha 21na kuwatunza watoto na kuwapatia malezi bora na siyo kuwatelekeza na kubaki mitaani wakilandalanda hovyo na kujilea wenyewe kwa kuomba omba.

Katika hatua nyingine, ameitaka jamii kujenga utamaduni wa kuandika Wosia wangali bado hai, ili kuondoa Migogoro ya Mirathi pale watakapo fariki dunia, na kuziacha familia zikiendelea kuwa na Amani.

Akizungumzia suala la utunzaji wa Mazingira, amewataka wananchi wasifumbie macho uchafuzi wowote wa mazingira sababu kuishi katika mazingira safi ni haki yao kisheria.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Mpomvu Mathias Samweli, amepongeza utolewaji wa elimu ya msaada huo wa kisheria, na kuwataka wananchi pale wanapokuwa na Migogoro wasijichukulie sheria mkononi, bali watumie sheria kutatua matatizo yao.

Mwanasheria na Afisa Miradi kutoka (LEAT) Clay Mwaifani akitoa elimu ya msaada wa kisheria kwa wanananchi wa Mpomvu Geita.

Wakili Teresia Fabia kutoka (LEAT) akitoa elimu ya msaada wa kisheria kwa Wananchi wa Mpomvu Geita.

Mkurugenzi kutoka Taasisi ya msaada wa Kisheria  Geita (GELAC) Elyneema Mafie akitoa elimu ya msaada wa kisheria kwa wananchi.

Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Mpomvu Kabula Sita akizungumza kwenye Mkutano huo wa utolewaji wa elimu ya msaada wa kisheria.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Mpomvu Mathias Samweli akizungumza kwenye Mkutano huo wa utolewaji wa elimu ya msaada wa kisheria.

Wananchi wa Mpomvu wakisikiliza elimu ya msaada wa kisheria.

Viongozi wa Mtaa wa Mpomvu wakisikiliza elimu ya msaada wa kisheria.
Wananchi wa Mpomvu wakisikiliza elimu ya msaada wa kisheria.
Wananchi wakiuliza maswali ya kisheria.
Wananchi wakiendelea kuuliza Maswali ya kisheria.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post