BODI YA EWURA YAKAGUA MIUNDOMBINU YA MAJI MZAKWE


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi EWURA( wa tatu kutoka kushoto mwenye fimbo) Prof. Mark Mwandosya akiwa juu ya tenki la kuhifadhi maji eneo la Mzakwe Dodoma, wakati wa ukaguzi wa miundombinu hiyo leo. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya DUWASA, Mhe. Davis Mwamfupe na wa pilu kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA Mhandisi Aron Joseph.


Wajumbe wa Bodi ya EWURA na wajumbe wa Bodi ya DUWASA wakiwa ziarani chanzo cha maji Mzakwe, wakati wa ukaguzi wa miundombinu ya kuzalisha na kihifadhi maji ya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dodoma.

Wajumbe wa Bodi ya EWURA na Bodi ya DUWASA wakiwa katika chanzo cha maji Mzakwe ili kukagua na kujiridhisha kuhusu hali ya miundombinu ya kuzalisha na kuhifadhi maji

Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) leo, imekagua miundombinu ya kuzalisha na kuhifadhi maji ya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dodoma ( DUWASA) iliyopo eneo la Mzakwe, jijini Dodoma kwa lengo la kujiridhisha na hali ya upatikanaji wa huduma ya maji jijini Dodoma.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post