LEAT YAKUTANA NA WABUNGE KUJADILI SERA NA SHERIA ZINAZOHUSU SEKTA YA UZIDUAJI

Mkurugenzi Mtendaji kutoka Timu ya Wanasheria watetezi wa Mazingira kwa vitendo (LEAT)Dk. Rugemeleza Nshala akiwasilisha mada ya Sheria katika sekta ya uziduaji Mafuta, Gesi asilia na Madini kwenye mafunzo yao na wabunge ambao ni wadau wa mazingira.

Na Marco Maduhu, DODOMA

TIMU ya Wanasheria watetezi wa Mazingira kwa vitendo (LEAT) imekutana na wabunge ambao ni wadau wa madini na mazingira, kujadili kwa pamoja namna ya kuboresha Sera na Sheria zinazohusu Sekta ya uziduaji, Mafuta, Gesi asilia na madini.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Aprili 29,2023 Jijini Dodoma.

Akizungumza kwenye Mafunzo hayo Mkurugenzi mtendaji wa Timu ya Wanasheria watetezi wa Mazingira kwa vitendo (LEAT) Dk. Rugemeleza Nshala, amesema wamekutana na wabunge hao sababu wao ni watunga sheria, waone namna ya kuishauri Serikali ili Rasilimali za nchi zinufaishe watanzania na vizazi vijavyo.

Amesema baadhi ya vifungu katika sheria ya madini, vinapaswa kufanyiwa mabadiliko au maboresho ikiwamo na namna kuboresha mikataba ambayo nchi inaingia na makampuni ya uwekezaji kutoka nje ya nchi.

"LEAT tumekutana na wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi kujadili kwa pamoja Sera na Sheria zinazohusu Sekta ya uziduaji, sababu wao ni watunga sheria na wataishauri Serikali kupitia vikao vya Bunge na hatimaye nchi yetu itanufaika na Sekta hii ya uziduaji sababu ni Rasilimali ambazo zinakwisha,"amesema Dk. Nshala.

Nao baadhi ya wabunge ambao wanatoka kwenye maeneo ya uchimbaji wa madini akiwamo Mbunge wa Msalala Iddi Kassimu, amesema mkutano huo umekuwa na manufaa sana, sababu wamejadili kwa pamoja na kuongeza uelewa namna ya kuisaidia Serikali, ili nchi ipate kunufaika na Rasilimali zake kwa kuboresha Sera, Sheria, na mikataba.

Aidha, katika mkutano huo ziliwasilishwa mada mbalimbali, ikiwamo Sheria katika Sekta ya uziduaji, mabadiliko ya Sheria na athari zake kwenye mapato ya madini, changamoto wanazokutanazo wachimbaji wadogo, pamoja na ulinzi wa Mazingira na haki za ardhi.
 Mkurugenzi Mtendaji kutoka Timu ya Wanasheria watetezi wa Mazingira kwa vitendo (LEAT)Dk. Rugemeleza Nshala akiwasilisha mada ya Sheria katika Sekta ya uziduaji Mafuta, Gesi asilia na Madini kwenye mafunzo yao na wabunge ambao ni wadau wa mazingira
Mkurugenzi Mtendaji kutoka Timu ya Wanasheria watetezi wa Mazingira kwa vitendo (LEAT)Dk. Rugemeleza Nshala akiwasilisha mada ya Sheria katika sekta ya uziduaji Mafuta, Gesi asilia na Madini kwenye mafunzo yao na wabunge ambao ni wadau wa mazingira.
Mwezeshaji Silas Olang akiwasilisha mada ya mabadiliko ya sheria na athari zake kwenye mapato ya madini.
Mwezeshaji Evans Rubara akiwasilisha mada juu ya changamoto ambazo wanakumbana nazo wakichimbaji wadogo katika Sekta ya madini.
Clay Mwaifwani kutoka Timu ya Wanasheria watetezi wa Mazingira kwa vitendo (LEAT) akiwasilisha mada ya ulinzi wa Mazingira na haki za aridhi kwa wabunge ambao ni wadau wa madini na mazingira.
Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini Dustan Kitandula akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Mbunge wa Jimbo la Msalala Idd Kassim akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini Geofrey Mwambe akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Mbunge wa Jimbo la Taarime Vijijini Mwita Waitara akichagia mada kwenye mafunzo hayo.
Wabunge wakiendelea kuchangia mada kwenye mafunzo hayo.
Wabunge wakiendelea kuchangia mada kwenye mafunzo hayo.
Wabunge wakiendelea kuchangia mada kwenye mafunzo hayo.
Wabunge wakiendelea kuchangia mada kwenye mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea kwa wabunge ambao ni wadau wa madini na mazingira.

Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea kwa wabunge ambao ni wadau wa madini na mazingira.
Mafunzo yakiendelea kwa wabunge ambao ni wadau wa madini na mazingira.
Mbunge wa jimbo la Masasi Mjini Geofrey Mwambe.
Wabunge wakiendelea na mafunzo.
Wabunge wakiendelea na mafunzo.
Wabunge wakiendelea na mafunzo.
Wabunge wakiendelea na mafunzo.
Wabunge wakiendelea na mafunzo.
Wabunge wakiendelea na mafunzo.
Wabunge wakiendelea na mafunzo.
Mbunge wa Taarime Vijijini Mwita Waitara akiwa kwenye mafunzo.
Wabunge wakiendelea na mafunzo.
Wawezeshaji wa mafunzo kwa wabunge.
Timu ya Wanasheria watetezi wa Mazingira kwa vitendo LEAT wakifuatilia mafunzo.
Picha ya pamoja ikipigwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments