SHINYANGA YAPANDA MITI KUELEKEA MAADHIMISHO YA MIAKA 59 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR KATIKA SHULE MPYA YA SEKONDARI YA WASICHANA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akipanda mti katika shule mpya ya Sekondari ya Wasichana iliyopo Butengwa Manispaa ya Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Mkoa wa Shinyanga umepanda miti katika shule mpya ya Sekondari ya wasichana iliyopo Butengwa Manispaa ya Shinyanga katika kuelekea maadhimisho ya  miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Zoezi hilo la upandaji miti limefanyika leo Aprili 25, 2023 na kuhudhuliwa na wananchi, wanafunzi, na watumishi wa Serikali, na kuongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, ambapo maadhimisho hayo Kimkoa na Kitaifa yatafanyika kesho.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo la upandaji miti  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amewataka Watanzania kuwapuuza watu ambao wamekuwa wakiubeza Muungano, akieleza kwamba hawajui faida yake ikiwa ni moja ya kichocheo cha kudumisha Amani.

Amesema Muungano ni mzuri na ndiyo umemtoa hata Rais Samia, na amewakuwa akifanya mambo mazuri ya kuletea maendeleo Watanzania, na kuwataka wananchi kuendelea kuuenzi.

Katika hatua nyingine amewataka wananchi wa Mkoa huo zikiwako na Taasisi za Serikali, kuendelea kupanda miti kwa wingi ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kuondoa hali ya ukame iliyopo katika Mkoa huo, huku akiwaonya pia kuacha tabia ya kukata miti hovyo.

Pia amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote sita mkoani humo, kuhakikisha wanatekeleza agizo la Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kwa kupanda Miti milioni 1.5 kila mwaka.

Naye Meya wa Manispaa ya Shinyanyanga Elias Masumbuko, amesema katika Manispaa hiyo wamekuwa wakijitahidi kupanda miti kutekeleza agizo la Makamu wa Rais, na mwaka huu wameshapanda miti zaidi ya laki moja na kubainisha zoezi hilo la upandaji miti ni endelevu.

Afisa Maliasili na Mazingira Mkoa wa Shinyanga Angela Erasmu, amesema wamekuwa wakiendesha kampeni mbalimbali za upandaji miti mkoani humo, na kutaja takwimu kwamba kuanzia Novemba mwaka jana hadi April mwaka huu imeshapandwa jumla ya miti milioni 4.6 kwa Mkoa mzima.

Ametaja baadhi ya sababu ambazo zimekuwa zikisababisha miti ambayo inapandwa kutokua, ni mifugo kula miti hiyo pamoja na hali ya ukame.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akijiandaa kupanda Mti katika Shule Mpya ya Sekondari ya wasichana iliyopo Butengwa Manispaa ya Shinyanga katika kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akipanda Mti katika Shule Mpya ya Sekondari ya wasichana iliyopo Butengwa Manispaa ya Shinyanga katika kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mkuu wa wialaya ya Shinyanga Johari Samizi akipanda Mti katika Shule Mpya ya Sekondari ya wasichana iliyopo Butengwa Manispaa ya Shinyanga katika kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi akipanda Mti katika Shule Mpya ya Sekondari ya wasichana iliyopo Butengwa Manispaa ya Shinyanga katika kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akipanda Mti katika Shule Mpya ya Sekondari ya wasichana iliyopo Butengwa Manispaa ya Shinyanga katika kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akipanda Mti katika Shule Mpya ya Sekondari ya wasichana iliyopo Butengwa Manispaa ya Shinyanga katika kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Shinyanga Lucas Mzungu akipanda Mti katika Shule Mpya ya Sekondari ya wasichana iliyopo Butengwa Manispaa ya Shinyanga katika kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Zoezi la upandaji miti likiendelea katika kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga Emmael Nkopi akipanda miti katika kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Zoezi la upandaji miti likiendelea katika kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Zoezi la upandaji miti likiendelea katika kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Zoezi la upandaji miti likiendelea katika kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Zoezi la upandaji miti likiendelea katika kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Zoezi la upandaji miti likiendelea katika kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Zoezi la upandaji miti likiendelea katika kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Zoezi la upandaji miti likiendelea katika kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Zoezi la usafi wa mazingira likiendelea katika Shule mpya ya Sekondari ya wasichana iliyopo Butengwa katika kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments