SIMBA SC YAICHAKAZA YANGA KWA MKAPA... INONGA, KIBU WALETA SHANGWE

SIMBA SC wameendelea kupunguza gape la Pointi dhidi ya Yanga SC na kuendelea na mbio za Ubingwa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Simba SC walianza kwa kasi ya ajabu na mnamo dakika ya 2 Beki Kisiki Henock Inonga aliwanyanyua mashabiki wake akifunga bao safi kwa kichwa akimalizia Krosi ya Shomari Kapombe.

Baada ya kupata bao hilo Simba waliendelea kuishambulia Yanga na dakika ya 32 Kiungo mshambuliaji aliyekubarika kwa mashabiki Kibu Denis alipigilia msumari wa pili kwa shuti kali lililomshinda Diarra.

Kwa ushindi huo Simba wamefikisha Pointi 63 na kupunguza gape la Pointi na kubaki alama tano huku kila timu ikibakiwa na mechi nne Ligi imalizike.


Yanga wanabaki na Pointi zao 68 ili wawe mabingwa wa Ligi msimu huu wanahitaji kushinda mechi tatu ili wafikishe Pointi 76 ambazo Simba akishinda mechi zake zote atakomea pointi 75 .


Chanzo - Mzalendo blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post