BENKI YA CRDB YAWAPA SOMO WANAFUNZI WA CHUO KIKUU DODOMA


Kaimu Mkuu wa Kitengo cha mafunzo na uendelezaji wa wafanyakazi benki ya CRDB Edith Muyombela akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) alipoelezea huduma zinazotolewa na benki hiyo lililofanyika Aprili 01,2023 katika ukumbi wa CIVE Auditorium chuoni hapo Jijini Dodoma
Benki ya CRDB kwa imeshiriki katika Kongamano la kuwajengea uwezo wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiuongozi pindi wamalizapo masomo, lililofanyika Aprili 01,2023 katika ukumbi wa CIVE Auditorium chuoni hapo.



Benki ya CRDB imekuwa ni moja ya benki kiongozi nchini katika kuhakikisha inashiriki kuelimisha makundi ya vijana wa vyuo mbalimbali nchini kupitia program mbalimbali yakiwemo Mafunzo kwa vitendo ‘Field attachmets’, Mafunzo kazini 'Ínternship’ na Programu maalumu ya Maendeleo ya wahitimu ‘Apprenticeship’ ambayo yalianzishwa mwaka 2020 kwa kuwachukua wahitimu 29 kutoka nchini Tanzania na 2 kutoka nchini Burundi.


Pia Benki ya CRDB kila mwaka huchukua kati ya wanafunzi 300 hadi 500 na kuwaunganisha katika vitengo mbalimbali vilivyopo ndani ya benki hiyo na kwenye matawi yake yaliyosambaa kote nchini ilikuweza kuwapatia mafunzo ya vitendo.


Kongamano hilo lililohudhuriwa na Mkurungenzi wa Elimu ya Juu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia ,Dk Kenedy Hosea, Benki ya CRDB iliwakilishwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha mafunzo na uendelezaji wa wafanyakazi, Edith Muyombela.


Wanafunzi wa vyuo nchini wamekuwa wakifurahia huduma mbalimbali za kibenki kutoka Benki ya CRDB ikiwa ni pamoja na upatikananji wa mikopo maarufu kama Boom Advance umekuwa ni mkombozi kwa wanafunzi wengi wanaotumia benki ya CRDB kwakujipatia mikopo rahisi hivyo kurahisisha kukabiliana na changamoto mbalimbali za kifedha.


Pia Benki ya CRDB imewatengenezea akaunti maalumu ya wanafunzi wa vyuo ambayo gharama zake za kufungua akaunti hiyo ni shilingi za Kitanzania Elfu Tano tu (5,000). wastani wa mikopo 20,000 inatolewa kila Mwezi kwa wanafunzi mbalimbali nchini, na wastani wa akaunti 50,000 zinafunguliwa kila mwaka na wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu nchini.


Kwa miaka kadhaa, Benki ya CRDB imekuwa Mshirika wa Umoja wa Taasisi za Elimu ya juu za wanafunzi nchini Tanzania ‘AIESEC’.

Mkurungenzi wa elimu ya Juu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia ,Dk Kenedy Hosea (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Wafanayakazi wa Benki ya CRDB kuhusu huduma zinazotolewa na benki hiyo alipotembelea banda la CRDB Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) lililofanyika Aprili 01,2023 katika ukumbi wa CIVE Auditorium chuoni hapo Jijini Dodoma Kaimu Mkuu wa Kitengo cha mafunzo na uendelezaji wa wafanyakazi benki ya CRDB .Edith Muyombela akiwa kwenye Banda la CRDB ambapo walikua wakielezea kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) huduma zinazotolewa na benki hiyolililofanyika Aprili 01,2023 katika ukumbi wa CIVE Auditorium chuoni hapo Jijini Dodoma

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments