MWILI WA MWANAUME WALIWA NA FISI KICHAKANI


Mnyama Fisi

Familia moja eneo la Juja inalia kifo cha mpendwa wao aliyeshambuliwa na fisi hadi kufariki dunia.

Kwa mujibu wa wakazi, waliamkia mabaki ya mwili uliokuwa umevamiwa na wanyama hao huku mzoga tu ukibaki.

Tukio hilo lilifanyika kijiji cha Canaan, Mastore Juja Ijumaa Machi 3,2023 kwani wakazi walipata mabaki hayo Jumamosi.

 "Umepatikana katika kichaka kilicho eneo hili lakini bado haujatambulika," mkazi aliyeshuhudia alisema.

Eneo hilo hujulikana kwa kuwa na wanyama hao ambao hutishia wakazi pakubwa kutokana na mashambulizi yake.

Aidha baadhi walisema haijabainika iwapo mauaji yalitekelezwa kwa mwathiriwa kabla ya mwili wake kutupwa ili uliwe na wanyama hao hatari.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post