MISAADA ILIYOTOLEWA NA SERIKALI YA TANZANIA KWA WAHANGA WA KIMBUNGA FREDDY YAVUKA MPAKA KUELEKEA MALAWI






Na Mwandishi wetu,OWM.


MKURUGENZI Msaidizi  anayeshughulikia Operesheni pamoja na Uratibu wa shughuli za Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Luteni Kanali Selestine Masalamado ameongoza ujumbe wa kutoka Nchini Tanzania kupeleka misaada ya unga, mahindi, mablanketi, mahema na madawa mbalimbali ambayo yatasaidia wahanga wa Kimbunga Freddy kilichotokea nchini Malawi.

Luteni Kanali Masalamado amesema hayo wakati Msafara wa magari ya jeshi la Wanachi wa Tanzania yakivuka mpaka wa Kasumulu wilaya ya Kyela kuelekea Mji wa Blantyre Nchini Malawi tarehe 22/03/2023.

“Natoa pole kwa ndugu zetu, wananchi wa Malawi tuko nao katika hali hii ngumu,” alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa kikosi Luteni Kanali George Kamya amesema wanasikitika kwa yale yaliyotokea nchini Malawi baada ya kupigwa na Kimbunga Freddy.

“Katika kuitikia hilo serikali ya Tanzania imetoa msaada kuwasaidia wenzetu waliopata na haya Majanga,” alisema

Kwa upande wake Mkuu wa Msafara Luteni Kanali George Kamya amesema wanasikitika kwa yale yaliyotokea nchini Malawi baada ya kupigwa na Kimbunga Freddy.

“Katika kuitikia hilo serikali ya Tanzania imetoa msaada kuwasaidia wenzetu waliopata na haya Majanga,” amesema

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Karonga Nchini Malawi Mhe. Roderick Mateauma ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusema kwamba msaada huo utasaidia kupunguza athari kwa wahanga na inaonesha mahusiano ya karibu yalipo kati ya nchi hizo mbili.

 

  

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments