MCHECHU AKABIDHIWA RASMI OFISI YA MSAJILI WA HAZINA, AANZA MAJUKUMU YAKE

Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu ameanza rasmi majukumu yake baada ya kukabidhiwa ofisi na mtangulizi wake, Mgonya Benedicto jana katika Ofisi ya Msajili wa Hazina, Dar es Salaam. Mchechu ameteuliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni na Mheshimiwa Rais Samia Saluhu Hassan. Kabla ya uteuzi huo, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika na Nyumba la Taifa (NHC).
Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Ofisi ya Msajili wa Hazina jana mara baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi.
Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu akizungumza na Menejimenti ya Ofisi ya Msajili wa Hazina jana baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi na mtangulizi wake, Mgonya Benedicto.


(Picha na Ofisi ya Msajili wa Hazina)Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments