MAMENEJA 126 SACCOS WAJIFUNGIA KWA SIKU 4 JIJINI DODOMA KUJADILIANA NAMNA BORA KUVISIMAMIA VYAMA VYA USHIRIKA


NAIBU Mrajis wa Vyama vya Ushirika - Udhibiti Bw. Collins Nyakunga,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Nne wa Meneja wa Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania kilichofanyika leo Machi 14,2023 jijini Dodoma.


Mrajis Msaidizi wa Vyama vya kifedha kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Josephat Kisamalala, akiwasilisha taarifa ya Usimamizi na Uendeshaji wa SACCOS wakati wa Mkutano wa Nne wa Meneja wa Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania kilichofanyika leo Machi 14,2023 jijini Dodoma.


SEHEMU ya Washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika - Udhibiti Bw. Collins Nyakunga (hayupo pichani) ,wakati akifungua Mkutano wa Nne wa Meneja wa Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania ulioanza leo Machi 14,2023 jijini Dodoma.


MTENDAJI Mkuu Sccult (1992) Ltd Bw.Hassani Mnyone,akizungumza wakati wa Mkutano wa Nne wa Meneja wa Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania ulioanza leo Machi 14,2023 jijini Dodoma.


KAIMU Msaidizi Mkoa wa Dodoma Octavian Bidyanguze,akitoa salamu za Mkoa kwa washiriki wa Mkutano wa Nne wa Meneja wa Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania ulioanza leo Machi 14,2023 jijini Dodoma.


MWENYEKITI wa Jukwaa Bosco Simba,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki mara baada ya Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika - Udhibiti Bw. Collins Nyakunga,wakati akifungua Mkutano wa Nne wa Meneja wa Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania kilichofanyika leo Machi 14,2023 jijini Dodoma.

Mrajis wa Vyama vya Ushirika - Udhibiti Bw. Collins Nyakunga,akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki mara baada ya kufungua Mkutano wa Nne wa Meneja wa Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania uliofanyika leo Machi 14,2023 jijini Dodoma.


Mrajis wa Vyama vya Ushirika - Udhibiti Bw. Collins Nyakunga,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua Mkutano wa Nne wa Meneja wa Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania uliofanyika leo Machi 14,2023 jijini Dodoma.


MENEJA Mkuu Bandarini Saccos Ltd Bw.Godfrey Rwehumbiza ,akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Mkutano wa Nne wa Meneja wa Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania kilichofanyika leo Machi 14,2023 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

MAMENEJA 126 wa Vyama vya Ushirika wa akiba na mikopo (SACCOS) wamejifungia kwa siku nne Jijini Dodoma kujadiliana namna bora ya kuvisimamia vyama vya ushirika na kuhakikisha wanaondoa hati chafu.

Akizungumza katika mkutano mkuu wa nne (4) wa Maneja hao uliofanyika leo Machi 14,2023,Jijini hapa,Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika, Udhibiti,Collins Nyakunga amesema nia ya jukwaa hilo ni kukumbushana,kubadilishana uzoefu, majukumu na namna bora ya kusimamia vyama vya ushirika.

“Tumeanza leo tutakaa kwa siku nne na tutabadilisha uzoefu namna kusimamia vyama vya ushirika na jinsi ya kufanya kwa kuzingatia weledi pamoja na kuzingatia maelekezo.

“Tunawakumbusha wajibu wao wa kila siku kuhakikisha wanatekeleza malengo yaliyokusudiwa na wanachama pamoja na kuhakikisha wanapata hati safi pamoja na kuzishauri vizuri bodi,”amesema

Aidha,Bw.Nyakunga amesema wapo mbioni kuanzisha benki ya ushirika na hivi karibuni watakutana kujadiliana namna bora ya kuweza kupata fedha.

Amesema mara baada ya sheria ndogo ya fedha kupitishwa hali ya vyama vya ushirika imezidi kuboreka huku akiishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuzidi kuwekeza kwenye mifumo ya tehama.

“Tunaona mabadiliko ni makubwa mameneja wanahamasika kusimamia hivi vyama lakini sasa hivi mambo yapo vizuri na tehema inasaidia ufanyaji kazi,kila kitu tunakiona na kila kinachofanyika tunakiona”amesema Nyakunga

Hata hivyo, ameiomba Serikali iendelee kuwaamini na wao wataendelea kusimamia mifumo kuhakikisha vyama vya ushirika vinaendelea kuiletea nchi maendeleo.

Kwa upande wake,Mrajis Msaidizi Vyama vya Ushirika wa kifedha kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TPDC) Joseph Kisamalala amewaomba mameneja kutumia mkutano huo kujadiliana changamoto mbalimbali ambazo zipo katika saccos.

“Niwapongeza tulivyoanza ilikuwa changamoto lakini sasa hivi sekta imekuwa tunaendelea kuwa imara zaidi na kuwa bora zaidi,”amesema Kisamalala.

Naye,Meneja Mkuu wa Bandarini Saccos Ltd,Godfrey Rwehumbiza amesema zaidi ya watu milioni 2 wameweza kupata huduma za kifedha kupitia Saccos mbalimbali.

“Niendelee kutoa wito Saccos nyingi kujitokeza na kuachana na changamoto kama zipo.Sisi kama Saccos tunashiriki kuhakikisha tunafikisha huduma na kutoa elimu wezeshi ili wananchi waweze kukopa,”amesema Rwehumbiza

Rwehumbiza amesema Mameneja wamebeba dira kuhakikisha mazuri yaliyopo katika saccos yanatajwa na kusemwa kuliko yale mabaya ambayo yamekuwa yakipaziwa sauti.

“Tunaona kwamba ni kitu kikubwa tunafanya katika jamii na sisi tutaendelea kuhamaisha ili waweze kupata manufaa, wito saccos nyingi zijitokeze ili kurahisha mchakato wa kujadili kuhusu maisha ya watanzania,”amesema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post