MAJALIWA-SUALA LA UHIFADHI VYANZO VYA MAJI NI MUHIMU, DAWASA ISIMAMIE SUALA HILI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akibonyeza kitufe kuzindua Mradi wa Ujenzi wa Mfumo wa Maji kati ya Makongo mkoani Dar es salaam na Bagamoyo Mkoani Pwani na Wiki ya Maji , leo Machi 16, 2023 Jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Mbatilo) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa DAWASA, Kiula Makala Kingu (wa tatu kulia) wakifurahia baada ya Waziri Mkuu kuzindua Mradi wa Ujenzi wa Mfumo wa Maji kati ya Makongo mkoani Dar es salaam na Bagamoyo Mkoani Pwani na Wiki ya Maji , Machi 16, 2023.(Picha na Emmanuel Mbatilo)Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikinga maji kwa mkono wakati alipozindua Mradi wa Ujenzi wa Mfumo wa Maji kati ya Makongo mkoani Dar es salaam na Bagamoyo Mkoani Pwani na Wiki ya Maji, kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Tegeta A Jijini Dar es Salaam, Machi 16, 2023.(Picha na Emmanuel Mbatilo)Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasili katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa Mfumo wa Maji kati ya Makongo mkoani Dar es salaam na Bagamoyo Mkoani Pwani na Wiki ya Maji , leo Machi 16, 2023 Jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Mbatilo) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasili katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa Mfumo wa Maji kati ya Makongo mkoani Dar es salaam na Bagamoyo Mkoani Pwani na Wiki ya Maji , leo Machi 16, 2023 Jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Mbatilo)Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Mradi wa Ujenzi wa Mfumo wa Maji kati ya Makongo mkoani Dar es salaam na Bagamoyo Mkoani Pwani na Wiki ya Maji, kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Tegeta A Jijini Dar es Salaam Machi 16, 2023. (Picha na Emmanuel Mbatilo) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Mradi wa Ujenzi wa Mfumo wa Maji kati ya Makongo mkoani Dar es salaam na Bagamoyo Mkoani Pwani na Wiki ya Maji, kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Tegeta A Jijini Dar es Salaam Machi 16, 2023. (Picha na Emmanuel Mbatilo)Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Maji Jumaa Aweso baada ya kuwasili katika hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa Mfumo wa Maji kati ya Makongo mkoani Dar es salaam na Bagamoyo Mkoani Pwani na Wiki ya Maji , leo Machi 16, 2023 Jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Mbatilo) Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa Mfumo wa Maji kati ya Makongo mkoani Dar es salaam na Bagamoyo Mkoani Pwani na Wiki ya Maji , leo Machi 16, 2023 Jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Mbatilo) Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Cprian Luhemeja akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa Mfumo wa Maji kati ya Makongo mkoani Dar es salaam na Bagamoyo Mkoani Pwani na Wiki ya Maji , leo Machi 16, 2023 Jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Mbatilo) Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa Mfumo wa Maji kati ya Makongo mkoani Dar es salaam na Bagamoyo Mkoani Pwani na Wiki ya Maji , leo Machi 16, 2023 Jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Mbatilo)Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa Mfumo wa Maji kati ya Makongo mkoani Dar es salaam na Bagamoyo Mkoani Pwani na Wiki ya Maji , leo Machi 16, 2023 Jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Mbatilo) Viongozi wa dini wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa Mfumo wa Maji kati ya Makongo mkoani Dar es salaam na Bagamoyo Mkoani Pwani na Wiki ya Maji , leo Machi 16, 2023 Jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Mbatilo) Baadhi ya Viongozi mbalimbali wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa Mfumo wa Maji kati ya Makongo mkoani Dar es salaam na Bagamoyo Mkoani Pwani na Wiki ya Maji , leo Machi 16, 2023 Jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Mbatilo) Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa Mfumo wa Maji kati ya Makongo mkoani Dar es salaam na Bagamoyo Mkoani Pwani na Wiki ya Maji , leo Machi 16, 2023 Jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Mbatilo) Baadhi ya wananchi wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa Mfumo wa Maji kati ya Makongo mkoani Dar es salaam na Bagamoyo Mkoani Pwani na Wiki ya Maji , leo Machi 16, 2023 Jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Mbatilo) Msanii wa Muziki wa Singeli, Shoro Mwamba akitumbuiza katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa Mfumo wa Maji kati ya Makongo mkoani Dar es salaam na Bagamoyo Mkoani Pwani na Wiki ya Maji , leo Machi 16, 2023 Jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Mbatilo) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Dini katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa Mfumo wa Maji kati ya Makongo mkoani Dar es salaam na Bagamoyo Mkoani Pwani na Wiki ya Maji , leo Machi 16, 2023 Jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Mbatilo) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa Mfumo wa Maji kati ya Makongo mkoani Dar es salaam na Bagamoyo Mkoani Pwani na Wiki ya Maji , leo Machi 16, 2023 Jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Mbatilo)

********************

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema suala uhifadhi wa mazingira ni muhimu kwa nchi na akataka kila Mtanzania azingatie uhifadhi wa mazingira.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Alhamisi, Machi 16, 2023) wakati akizungumza na wadau mbalimbali wa sekta ya maji na mamia ya wananchi waliohudhuria uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa Mfumo wa Usambazaji Maji kati ya Makongo na Mji wa Bagamoyo uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Tegeta A, jijini Dar es Salaam. Pia alizindua Wiki ya Maji kwa mwaka 2023.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema licha ya juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali za kuboresha miundombinu ya ukusanyaji na usambazaji wa maji, ni jukumu la kila Mtanzania kutunza vyanzo vya maji. “Tuna jukumu kubwa nalo ni la kutunza na kuhifadhi vyanzo vya maji; na eneo hili tuna mgogoro mkubwa kwani vyanzo vyetu vya maji vinaharibiwa, ni wajibu wetu kutunza vyanzo hivi.”

Amesema Mheshimiwa Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango ameshatoa mwongozo wa uhifadhi wa vyanzo vya maji na kila Mtanzania anapaswa kuzingatia hilo. “Tunahitaji kuweka nguvu moja katika kusimamia, kulinda, kuhifadhi na kuendeleza rasilimali za maji. Nitoe wito kwa Wizara, wadau wa maji na wananchi tutunze vyanzo hivi iwe ni visima, mito, au mifereji vyote tuvilinde.”

“Suala la uhifadhi ni muhimu sana. DAWASA isimamie suala hili kwa karibu na kutoa taarifa mapema. Wakurugenzi wa Mabonde ya Maji nchini kama vile Ruvuma, Rufiji, Malagarasi na mabonde mengine yote hakikisheni mnafanya ukaguzi wa mara kwa mara ili vyanzo hivi visiharibiwe. Wananchi tulinde vyanzo hivi na mtu akionekana anaharibu, kama ni kisima au chanzo kingine, tuchukue hatua, tusisite kwa sababu huo ni uhujumu.”

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na hadhira iliyokuwepo, Waziri wa Maji. Jumaa Aweso alimwagiza Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Bw. Kiula Kingu ahakikishe wananchi wote walioomba maji wafungiwe mita ndani ya siku saba kama Mkataba wa Huduma ya Wateja unavyosema.

Akielezea utekelezaji wa miradi ya maji kwenye wizara yake, Waziri Aweso alisema Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi kwenye wizara hiyo ambazo ni mahsusi kwa utekelezaji wa miradi ya maji. “Mheshimiwa Rais kwa sasa ametoa asilimia 90 ya fedha za utekelezaji wa miradi ya maji, wakati awali utekelezaji ulikuwa ni kati ya asilimia 50 hadi 60 tu,” alisema.

Alisema ili kukabiliana na uhaba wa maji, Wizara hiyo inapanga kujenga mabwawa kwenye maeneo mbalimbali ili kutengeneza akiba ya maji. Akitoa mfano, alisema Bwawa la Kidunda limeshapatiwa malipo ya awali ya sh. bilioni 49.

Akitoa maelezo kuhusu mradi huo katika eneo la Mivumoni, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Bw. Kiula Kingu alisema ujenzi wa mfumo wa usambazaji maji kutoka matenki ya DAWASA yaliyopo Chuo Kikuu cha Ardhi hadi Bagamoyo ni mradi wa kimkakati uliotekelezwa na Serikali kupitia DAWASA kwa kushirikiana na Benki ya Dunia.

“Mradi huu ambao umegharimu sh. bilioni 71.9 na kukamilika kwa asilimia 100, umelenga kuunganisha wateja wapya 35,000 na kwamba hadi sasa wateja 20,618 wamenufaika.

Alisema mradi huo umehusisha ujenzi wa matenki matatu makubwa yenye ujazo wa lita milioni tano kila moja, yaliyojengwa Vikawe, Mbweni na Tegeta A, ujenzi wa vituo viwili vya kusukuma maji vilivyojengwa eneo la Vikawe na Mbweni pamoja na ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji ndani ya eneo lote la mradi,” alisema.

Alisema maeneo yanayonufaika na mradi huo katika Wilaya ya Kinondoni ni kata za Changanyikeni, Vikawe, Goba, Mivumoni, Mbweni, Madale, Tegeta A, Bunju, Wazo, Ocean Bay na Salasala. Kwa upande wa Bagamoyo, kata zilizonufaika ni Mataya, Sanzale, Migude, Ukuni, Mtambani, Nianjema, Kimara ngo'mbe, Kisutu, Block P.

Kwa upande wa Vikawe, alizitaja kata zitakazonufaika na mradi huo kuwa ni Mapinga, kwa Matumbi na Vikawe bondeni. Kwa Mabwepande, ni kata za Bunju B, Mabwepande na Mbopo ilhali kata ya Salasala, mradi utahudumia Salasala, Kinzudi, Mbezi, Goba na Kilongawima.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bibi Preeti Arora alisema mradi huo ulilenga kuongeza upatikanaji wa maji na kwamba ameridhishwa kuona fedha zilizotolewa zinasimamiwa kwa karibu na Serikali ili kutimiza lengo lililokusudiwa.

Maadhimisho ya Wiki ya Maji yameanza leo Machi 16 na yatahitimishwa Machi 22, mwaka huu yakiwa na kaulimbiu isemayo: “Kuongeza Kasi ya Mabadiliko katika Sekta ya Maji kwa Maendeleo endelevu ya Uchumi.”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post