HAKIRASILIMALI WAMEENDESHA KONGAMANO LA WANAWAKE SEKTA YA UZIDUAJI

Kongamano la wanawake sekta ya Uziduaji, Mafuta,Gesi asilia na Madini likifanyika mkoani Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

TAASISI ya HakiRasilimali imeendesha Kongamano la Wanawake Sekta ya Uziduaji (Mafuta, Gesi asilia na Madini) kujadili changamoto na kuzitafutia ufumbuzi pamoja na fursa zilizopo ili wapate kunufaika na Mnyonyoro wa Thamani kwenye Sekta hiyo.

Kongamano hilo limefanyika leo Machi 7, 2023 mkoani Shinyanga na kushirikisha vyama mbalimbali vya wanawake wachimbaji wa madini, wadau wa madini, pamoja na Maofisa kutoka Tume na Wizara ya Madini, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kilele chake ni kesho.

Mkurugenzi wa HakiRasilimali Adam Anthony akizungumza kwenye Kongamano hilo, amesema wanawake wanapaswa kufahamu fursa nyingi ambazo zipo kwenye Sekta ya Uziduaji ikiwamo kutoa huduma kwenye Migodi (Local Content) na hatimaye kuinuka kiuchumi na kunufaika na Rasilimali za Nchi.

“HakiRasilimali tumeendesha Kongamano hili la wanawake ambao wanajishughulisha na Sekta ya Uziduaji, Mafuta, Gesi asilia na Madini, ili kuendesha mijadala ya kujadili fursa zilizopo kwenye Sekta ya Uziduaji, Changamoto, na ushiriki ukoje wa wanawake kuwezeshwa kiuchumi kupitia Migodi (Local Content) ili wanufaika Mnyororo wa thamani kwenye Sekta ya Uziduaji,”amesema Antony.

Naye Paulo Mikongoti kutoka HakiRasilimali, amesema kwa utafiti ambao wameufanya Tarime na Geita, ili kuona jinsi wanawake wanavyoshiriki kwenye Sekta ya Uziduaji katika Madini, wamebaini kuwepo na uchache wa wanawake kupata fursa za uwezeshwaji kiuchumi kupitia vikundi na huduma ambazo wanazitoa ni matunda na mboga na malipo yao huchukua muda mrefu kulipwa.

Aidha, Katibu wa Chama Cha Wanawake Wachimbaji wa Madini na uongezaji thamani ya madini (WIMO) Mhandisi Lightness Salema, amesema wanawake wanapaswa kushirikishwa vyema kwenye sekta ya Uziduaji ikiwamo kutengewa maeneo yao ya uchimbaji madini, pamoja na kuwezeshwa mitaji na vifaa, ili wafanye shughuli kubwa ambazo zitawainua kiuchumi.

Kaimu Meneja wa Tathimini na ufuatiliaji Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi Oswald Karadisi, amewataka wanawake wajiunge kwenye Kanzi Data ya Taifa ili kujua fursa mbalimbali zilizopo kwenye Sekta ya Uziduaji, pamoja na kufahamu mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ambayo ipo 73, mifuko 63 ya Serikali na 10 ni Sekta Binafsi, ambayo inatoa Ruzuku, mikopo ya moja kwa moja pamoja na dhamana.

Mgeni Rasmi kwenye Kongamano hilo Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi, amewapongeza wanawake kwa kujishughulisha na Sekta ya Uziduaji, kwamba Sekta hiyo ilikuwa ikiaminika kuwa ni ya wanaume lakini wao wameingia kwa miguu yote miwili.

“Sekta hii ni Pana sana, mimi niliingia na mguu mmoja lakini nyie mmeingia na miguu miwili na hapa mlipofikia nyie ni Super women,”amesema Samizi.

Amewataka pia viongozi waliopewa dhamana walisimamie suala la Local Content sababu lipo kisheria, huku akitoa wito kwa Tume ya Madini na Wizara ya Madini kuwashika mkono wanawake wachimbaji wa madini pamoja na kuwapatia mikopo zikiwamo na Taasisi za kifedha ili wapate mitaji na kuendeleza shughuli zao kwa ufanisi zaidi.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwenye Kongamano la Wanawake Sekta ya Uziduaji lililoandaliwa na HakiRasilimali.

Mkurugenzi wa HakiRasilimali Adam Anthony akizungumza kwenye Kongamano la Wanawake Sekta ya Uziduaji.

Paul Mikongoti kutoka HakiRasilimali akizungumza kwenye Kongamano la Wanawake Sekta ya Uziduaji.

Meneja wa Tathimini na ufuatiliaji Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi Oswald Karadisi, akizunguma kwenye Kongamano la Wanawake Sekta ya Uziduaji.

Geofrey Nsemwa kutoka Tume ya Madini Tanzania akizungumza kwenye Kongamano hilo la Wanawake Sekta ya Uziduaji.

Francis Mihayo kutoka Wizara ya Madini akizungumza kwenye Kongamano hilo la Wanawake Sekta ya Uziduaji.

Mratibu wa Mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania (WFT-Trust) mkoani Shinyanga Glory Mbia akizungumza kwenye Kongamano la Wanawake Sekta ya Uziduaji.

Wachokoza Mada kwenye Kongamano la Wanawake Sekta ya Uziduaji.

Kongamano la Wanawake Sekta ya Uziduaji likiendelea mkoani Shinyanga lililoandaliwa na HakiRasilimali.

Picha ya pamoja ikipigwa.

Picha ya pamoja ikipigwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments