MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI YAFANYIKA MWAMASHELE SHINYANGA...MKUDE AWAONESHA FURSA MTANDAONI

Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Mkoani Shinyanga

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MAADHIMISHO ya siku ya Wanawake Duniani Mkoani Shinyanga, yamefanyika katika Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu, huku wanawake wakitakiwa kupaza sauti za vitendo vya ukatili wa kijinsia, pamoja na kuchangamkia fursa ya Mikopo asilimia 10 kujikwamua kiuchumi.

Maadhimisho hayo yamefanyika leo Machi 8,2023 katika Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu mkoani Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo, viongozi wa Serikali, Chama, huku likiendana sambamba na utoaji wa mifano ya hundi katika vikundi vya wanawake wajasiriamali na utoaji wa Gesi za kupikia.

Akizungumza Mgeni Rasmi kwenye maadhimisho hayo Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amewataka wanawake mkoani humo kuchangamkia fursa za mikopo asilimia 10 ambazo zinatolewa na Halmashauri kupitia mapato ya ndani ili wapate shughuli za kufanya na kuinuka kiuchumi.

"Nawapongeza Wakurugenzi kwa kuendelea kutoa fedha za mikopo asilimia 10 kwa vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu na ninaomba vikundi ambavyo vinapewa fedha hizi za mikopo vifuatiliwe ili fikie malengo na kujikwamua kichumi," amesema Mkude.

"Nawaomba pia wanawake wajasiriamali katika utengenezaji wa bidhaa zenu, muwe wabunifu na kutengeneza bidhaa zenye ubora pamoja na kuzitangaza kupitia mitandao ya kijamii ili kuongeza masoko zaidi yakiwamo ya nje," ameongeza.

Katika hatua nyingine Mkude amewataka wanawake kupinga masuala ya Mila na Desturi zenye madhara ambazo zinakandamiza wanawake kupata fursa mbalimbali ikiwamo nafasi ya uongozi.

Pia alisisitiza wananchi wa mkoa wa Shinyanga kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya kujikinga na Maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi, ugongwa wa COVID-19 ikiwamo kupata Chanjo ya UVIKO-19, pamoja na kuwapaleka wa watoto kupata Chanjo ya pili ya Surua.

Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake mkoani Shinyanga Dk. Regina Malima, akisoma Risala ya Wanawake kwenye maadhimisho hayo, amesema changamoto ambazo zinawakabili wanawake ni ukosefu wa Rasilimali fedha, baadhi kuwa na uelewa mdogo masuala ya ujasiriamali, kushindwa kutumia fursa zikiwano za mikopo.

Ametaja Changamoto zingine ni ukosefu wa masoko ya mazao ambayo yanalimwa na wanawake.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale akisoma taarifa ya Mkoa amesema katika uwezeshaji wanawake kiuchumi kipitia fedha za mikopo kimeshatolewa kiasi cha fedha Sh.bilioni 2.5 kuanzia mwaka wa fedha 2022 hadi Machi 2023.

Aidha, Kauli Mbiu katika Maadhimisho hayo ni Ubinifu na Mabadiliko ya Teknolojia, chachu katika kuleta usawa wa kijinsia, huku Maadhimisho hayo yakihudhuliwa pia na Wabunge wa Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu.

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza kwenye kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwenye kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita akizungumza kwenye kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu.

Afisa Maendeleo mkoani Shinyanga Tedyson Ngwale akitoa taarifa ya Mkoa kwenye Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu.

Mwenyekiti wa Jukwaa la uwezeshaji wanawake mkoani Shinyanga Dk, Rejina Malima akisoma Risala ya wanawake kwenye Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu.

Katibu wa UWT mkaoni Shinyanga Asha Kitandala akizungumza kwenye Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu.

Mbunge wa Viti maalumu mkoani Shinyanga Christina Mzava akizungumza kwenye Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nice Munissy (kushoto) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita kwenye Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga.

Wanawake wakiwa kwenye Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kimkoa wa Shinyanga yamefanyika wilayani Kishapu Kata ya Mwanashele.

Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yakiendelea mkoani Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akitoa mfano wa hudi kwa vikundi vya ujasiriamali kupitia fedha za mikopo ya halmashauri asilimia 10 ya mapato ya ndani kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude (kushoto) akikabidhi Majiko ya Gesi kwa vikundi vya Mama Lishe wa Manispaa ya Shinyanga kwenye Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akikabidhi mifuko 45 ya Saruji kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye ujenzi wa Hosteli ya wasichana katika Shule ya Sekondari ya Mwamashele wilayani Kishapu kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Kishapy Joseph Mkude akiendelea kupokea Mifuko ya Saruji.

Awali Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akiwa katika Banda la Benki ya CRDB kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga.

Awali Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akiwa katika Banda la kituo cha Taarifa na Maarifa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyangaa akiangalia bidhaa mbalimbali ambazo wanatengeneza za Ujasiriamali.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akiwa kwenye Banda la Shirika la Rafiki SDO kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi (kushoto) akipiga picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nice Munissy (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa Kishapu Emmanuel Johnson kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post