WAOMBAJI NAFASI JWTZ WATAHADHARISHWA


Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Kanali Gaudentius Gervas Ilonda akitoa taarifa ya nafasi za kujiunga na Jeshi hilo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Machi 09, 2023 kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dodoma.


Na Dotto Kwilasa, DODOMA .

JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limewatahadharisha wananchi kuwa makini na matapeli pindi wanapoanza kutafuta ajira kwani kumekuwa na tabia ya kuibuka matapeli pindi matangazo ya nafasi za kujiunga na jeshi hilo zinapotangazwa.

Kaimu Mkurugenzi wa Habari na uhusiano wa JWTZ, Luteni Kanali Gaudentius Ilonda amesema hayo leo Machi 9,2023 Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa ya nafasi  za kujiunga na Jeshi kwa vijana wa kitanzania.

Akizungumzia uwepo wa nafasi hizo amesema vijana wenye elimu ya kuanzia kidato cha nne hadi shahada ya uzamili ambao wamemaliza mkataba wa mafunzo ya kujitolea JKT na kurudishwa majumbani ndiyo Wenye sifa za kuomba nafasi za kujiunga na Jeshi hilo.

"Natambua katika matangazo haya ya kujiunga na nafasi hizi kuna matapeli watajitokeza na kuanza kupenyeza utapeli wao ,mara jaza fomu hii kitu ambacho siyo kweli hivyo nawataka watanzania wasidanganyike wala kurubuniwa na hakuna njia ya mkato katika kupata nafasi hizi zaidi ya kuzingatia vigezo vilivywekwa wazi kabisa,'amesema.

Pamoja na hayo ametaka vijana hao watambue kwamba nafasi zinazotolewa  Matapeli hujitokeza  kutokana na kukua kwa teknolojia kila siku na kubuni mbinu mpya hivyo inabidi kuchukua tahadhari kwa pamoja ili kuepukana na mitego ya utapeli wao.

Aidha Luteni Kanali Ilonda amesema nafasi hizo zinawahusu vijana wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 26 kwa wenye elimu ya kidato cha 4 na cha sita na umri usiozidi miaka 27 kwa wenye elimu ya juu.

"Nafasi hizi haziwahusu vijana ambao bado wapo katika kambi mbalimbali za JKT kwa sasa bali zinawahusu wale ambao tayari wamemaliza mikataba yao ya mafunzo ya miaka miwili na kurudishwa majumbani na wenye vigezo vilivyotajwa vya kuomba nafasi hii," amesisitiza Luteni Kanali Ilonda

Aidha,Luteni Kanali Ilonda, ametaja vigezo vitakavyozingatiwa wakati wa maombi hayo kuwa mwombaji awe raia wa Tanzania wa kuzaliwa mwenye kitambulisho cha Taifa,awe na afya nzuri na akili timamu,awe na cheti halisi cha kuzaliwa,vyeti vya shule nav yeti vya taaluma.

Vigezo vingine ni pamojana na awe hajatumikia Jeshi la Polisi,magereza,Chuo cha Mafunzo au Kikosi maalumu cha kuzuia magendo na asiwe ameoa au kuolewa.

Ameeleza utaratibu wa  kutuma maombi kuwa maombi yote yaandikwe kwa mkono na yawasilishwe makao makuu ya jeshi hilo Dodoma kwanzia leo Machi ,9 hadi Machi 20, 2023 yakiwa na viambatanisho ambavyo ni nakala ya kitambulisho cha taifa au namba ya nida,nakala ya cheti cha kuzaliwa,vyeti vya shule na chuo,nakala cheti cha JKT na namba ya simu ya mkononi ya muombaji .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments