MAOFISA UGANI, WATENDAJI WA KATA KISHAPU WAPEWA PIKIPIKI, DC MKUDE ATAKA ZILETE TIJA

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akiendesha Pikipiki wakati wa zoezi la kuzikabidhi kwa Maofisa Ugani na Kata Halmashauri ya wilaya ya Kishapu.

Na Marco Maduhu, KISHAPU

MAOFISA Ugani na Watendaji wa Kata Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, wamepewa vitendea kazi Pikipiki, ambazo watazitumia kwenye shughuli za Kiserikali.

Zoezi la kukabidhi Pikipiki hizo limefanyika leo Machi 9, 2023 katika Ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM), ili kuona namna Serikali Chini ya Rais Samia Suluhu inavyotekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza wakati wa kukabidhi Pikipiki hizo, amewataka Maofisa Ugani kuwa Pikipiki hizo zikatumike kwa madhumuni yaliyokusudiwa ikiwamo kuleta tija kwenye Sekta ya Kilimo.

“Maofisa Ugani leo tumewakabidhi vitendea kazi Pikipiki hizi hatutategemea kusikia Mkulima ambaye hajatembelewa na kupewa elimu ya Kilimo cha kisasa, tunataka tuone mabadiliko kwenye Sekta ya Kilimo  kwa sababu hakuna visingizio tena vya usafiri, Rais Samia ametatua tatizo hilo na kujali watumishi wake hivyo msimwangushe,”amesema Mkude.

Aidha, amewataka pia Watendaji wa Kata kwamba Pikipiki ambazo wamepewa wakazitumie vizuri ikiwamo kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato.

Naye Katibu Tawala wa wilaya ya Kishapu Shadrack Kengese, amewataka Maofisa Ugani pamoja na Watendaji wa Kata, wanapokuwa wakiendesha Pikipiki hizo wazingatia pia matumizi ya usafiri wa Serikali na siyo kukutwa nazo mida ya usiku zikiwa bar.

Pia amemuagiza Mkuu wa Polisi wilaya ya Kishapu, kuwa Watumishi hao kabla ya kuanza matumizi ya Pikipiki hizo, wapewa kwanza mafunzo ya Sheria za Usalama Barabarani, huku akiwataka wale ambao hawana Leseni wazikate.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Emmanuel Johnson, amesema Wizara ya Kilimo imetoa Pikipiki 39 kwa Maofisa Ugani wilayani humo, na Pikipiki Nne za Watendaji wa Kata zimetolewa na Ofisi ya Rais (TAMISEM), huku Pikipiki nyingine 10 ambazo zilinunuliwa na Halmashauri wamewapatia pia Watendaji wa Kata.

Nao baadhi ya Maofisa Ugani akiwamo Tito Nzungu wa Kata ya Ndoleleji, ameipongeza Serikali kwa kuwapatia vitendea kazi na kuahidi Pikipiki hizo watazitumia kwa madhumuni yaliyokusudiwa, na kuleta tija kwenye sekta ya kilimo, kwa kuwatembelea wakulima muda wote na kutoa elimu ya kilimo cha kisasa na kuongeza uzalishaji.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza wakati wa kukabidhi Pikipiki kwa Maofisa Ugani na Watendaji wa Kata Halmashauri ya wilaya ya Kishapu.

Katibu Tawala wilaya ya Kishapu Shadrack Kengese akizungumza kwenye Makabidhiano ya Pikipiki kwa Maofisa Ugani na Kata Halmashauri ya wilaya ya Kishapu.

Katibu wa UWT wilaya ya Kishapu Maua Hassan akizungumza kwenye Makabidhiano ya Pikipiki kwa Maofisa Ugani na Watendaji wa Kata Halmashauri ya wilaya ya Kishapu.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Emmanuel Johnson akizungumza wakati wa kukabidhi Pikipiki kwa Maofisa Ugani na Kata Halmashauri ya wilaya ya Kishapu.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akikata utepe kwa ajili ya kukabidhi Pikipiki kwa Maofisa Ugani na Watendaji wa Kata Halmashauri ya wilaya ya Kishapu.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akikata utepe kwa ajili ya kukabidhi Pikipiki kwa Maofisa Ugani na Watendaji wa Kata Halmashauri ya wilaya ya Kishapu.

Katibu Tawala wa wilaya ya Kishapu Shadrack Nkengese akiendesha Pikipiki wakati wa zoezi la kuzikabidhi kwa Maofisa Ugani na Kata Halmashauri ya wilaya ya Kishapu.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Emmanuel Johnson akiendesha Pikipiki wakati wa zoezi la kuzikabidhi kwa Maofisa Ugani na Kata Halmashauri ya wilaya ya Kishapu.

Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Kishapu Joseph Swalala akiendesha Pikipiki wakati wa zoezi la kuzikabidhi kwa Maofisa Ugani na Kata Halmashauri ya wilaya ya Kishapu.

Pikipiki ambazo wamekabidhiwa Maofisa Ugani na Watendaji wa Kata Halmashauri ya wilaya ya Kishapu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post