MVUA YA UPEPO YAATHIRI MIUNDOMBINU YA UMEME KISHAPU...TANESCO YASEMA WIZI VIFAA VYA UMEME VIMECHANGIA


Na Sumai Salum - Kishapu

Meneja wa shirika la umeme wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Elias Turnbull amewataka wananchi wenye tabia ya kuiba vifaa vya miundombinu ya umeme kuacha mara moja kwani jambo hilo linasababisha kukosekana kwa huduma hiyo muhimu kwa jamii.

 Turnbull  ameyasema hayo leo Machi 10,2023 wakati akizungumza na Malunde 1 blog baada ya kukosekana kwa umeme kwa zaidi ya saa 20 akibainisha kutwa kutokana na wizi wa vifaa vya umeme jumla ya nguzo 10 zimedondoka jana jion majira ya saa 12 huko Ukenyenge kutokana na mvua iliyoambatana na upepo mkali.


"Huwa kuna nguzo kwenye kona zinazoshikiliwa na waya (Stayroad) na ndani yake kunakuwa na kifaa kwa ajili ya kuifanya nguzo isidondoke kirahisi, sasa baadhi ya wafugaji wamekuwa na tabia ya kukifungua na kukiiba kisha wanaenda kufungia sheli zao( jembe la ng'ombe) ndiyo maana upepo ukitokea tu hata kidogo nguzo huanguka hivyo baada ya nguzo hiyo kubwa kuanguka ikasababisha zingine 9 kulala pia",ameeleza.


Aidha ameongeza kuwa tayari timu tatu kutokea Tanesco Meatu, Kishapu na Shinyanga ziko eneo ya tukio kwa ajili ya kuhakikisha huduma hiyo muhimu inarejea haraka iwezekanavyo.


Amewataka wananchi wote kuwa walinzi wa miundombinu ya umeme kwani kuiba vifaa vya miundombinu ni kulipa shirika hasara na pia wanasababisha kusimama kwa shughuli za uzalishaji katika jamii husika.

Hata hivyo amesema TANESCO itachukua hatua kali za kisheria kwa watu watakaobainika kuharibu miundombinu ya umeme.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post