Picha : PAP YAENDESHA WARSHA YA MAFUNZO KWA WABUNGE JUU YA USIMAMIZI WA UHAMIAJI BARANI AFRIKA


Bunge la Afrika (Pan - African Parliament - PAP) limeendesha Warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo Wabunge wa  Bunge la Afrika juu ya Masuala ya Usimamizi wa Uhamiaji (Migration Governance) katika Bara la Afrika.

Warsha hiyo (Capacity building training workshop on labour migration governance and administration for members of Pan – African Parliament)  inafanyika leo Jumanne Machi 14,2023 na Machi 15,2023 katika Ukumbi wa Bunge la Afrika, Midrand Afrika Kusini. 

Miongoni mwa sababu zilizotajwa kusababisha ongezeko la watu kuhama nchi zao ni pamoja na ukosefu wa Kazi na Ajira kwa vijana  baada ya kuhitimu masomo ya Chuo katika nchi za Afrika hali inayochangia kuhamia maeneo ili kutafuta ajira.

Tazama matukio katika picha wakati wa warsha..... Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Washiriki wa Warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo Wabunge wa  Bunge la Afrika juu ya Masuala ya Usimamizi wa Uhamiaji (Migration Governance) katika Bara la Afrika wakipiga picha ya pamoja
Warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo Wabunge wa  Bunge la Afrika juu ya Masuala ya Usimamizi wa Uhamiaji (Migration Governance) katika Bara la Afrika ikiendelea
Wabunge kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaowakilisha katika Bunge la Afrika, Mhe. Toufiq Salim Turkey (kushoto, Mhe. Anatropia Theonest na Mhe. Ng’wasi Damas Kamani (kulia) wakiwa kwenye Warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo Wabunge wa  Bunge la Afrika juu ya Masuala ya Usimamizi wa Uhamiaji (Migration Governance) Barani Afrika iliyoandaliwa na Bunge la Afrika.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post